Home LOCAL SERIKALI YASITISHA UCHAPISHAJI WA GAZETI LA UHURU KWA SIKU 14.

SERIKALI YASITISHA UCHAPISHAJI WA GAZETI LA UHURU KWA SIKU 14.

 

Na: Redempta  Ndubuja.

Serikali imesitisha uchapishaji na usambazaji wa gazeti la Uhuru kwa muda wa siku 14 kuanzia Agosti 12, 2021 kutokana na kutoa taarifa za uongo dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zilizochapishwa kwenye gazeti hilo yenye kichwa cha Habari, “Sina Wazo Kuwania Urais 2025- Samia.

Uamzi huo umetolewa leo Jijini Dodoma na Mkurugenzi wa  Idara ya Habari -MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa .

“Habari hii ina upungufu wa kisheria na weledi wa taaluma ya uandishi wa habari kwa kutoa taarifa za uongo dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Samia Suluhu Hassan , kinyume na kifungu cha 50 [1][ a],[b]na [d] na kifungu cha 52 [d] na [e] vya Sheria ya Huduma za Habari Na.12 ya 2016. Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan hajatoa matamshi yoyote ambayo yanaeleza kutokuwa na wazo la kuwania urais Mwaka 2025,

“Kwa mujibu wa kifungu cha 10[1] cha Sheria ya Huduma za Habari Na.12 ya 2016 ikiwa gazeti la Uhuru   halitaridhika na uamuzi wa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Habari linayo haki ya kukata rufaa kwa Waziri mwenye dhamana ya habari ,”alisema Msigwa.

Aidha, Msigwa amesema Idara ya Huduma za Habari inaamini kuwa adhabu hii itatoa nafasi ya kurekebisha masuala ya yanayohusu weledi wa Uandishi wa Habari na Utekelezaji wa masuala  yote yanayohusu uzingatiaji wa sheria , maadili na kanuni kwa  gazeti hilo.

Vilevile, Msigwa ametoa wito kwa vyombo vya habari vyote  kuhakikisha vinazingatia Sheria, maadili kanuni na miongozo mbalimbali inayohusu tasnia ya habari ili kulinda taaluma na kuleta ustawi wa jamii.

Mwisho.

 

Previous articleUMOJA WA AFRIKA KUIPATIA TANZANIA CHANJO MILIONI 17 ZA UVIKO 19
Next articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 12-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here