Home LOCAL RC MAKALLA: MWENGE KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM KUZINDUA MIRADI YA...

RC MAKALLA: MWENGE KATIKA MKOA WA DAR ES SALAAM KUZINDUA MIRADI YA SHILINGI BILIONI 105.

 

 

DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo August 18 amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo Uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ukitokea Mkoa wa Pwani na kuukabidhi kwa Wilaya ya Ilala kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya miradi ya maendeleo.

Akipokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Aboubakar Kunenge, RC Makalla amesema kwa siku tano ambazo  Mwenge wa Uhuru utakuwa Dar es salaam utapitia miradi ya maendeleo 46  yenye thamani ya Shillingi Billion 105.1.

Mwenge wa Uhuru umeanza rasmi kukimbizwa leo Mkoa wa Dar es salaam kwa kuanzia Wilaya ya Ilala Kisha Ubungo, Kinondoni, Kigamboni na Temeke ambapo ifikapo August 23 Mwenge huo utakabidhiwa kwa Mkoa wa Lindi ukienda na kaulimbiu inayolenga kuhimiza Matumizi sahihi ya TEHAMA.

Previous articleMAAFISA USTAWI WATAKIWA KUWAJIBIKA KUSAIDIA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI
Next articleWAZIRI MKUU AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI KUU CCM WILAYA YA RUANGWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here