– Ni sehemu mkakati wake wa kuwafikishia wananchi msaada wa kisheria kwenye maeneo yao.
– Awaalika Wenye Migogoro kuwasilisha kero zao.
– Asema kila mmoja atapata haki yake kwa mujibu wa Sheria.
– Awaandaa wataalamu wa sekta mbalimbali kwaajili ya kuhudumia kila atakaefika.
Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla anatarajiwa kuanza rasmi ziara ya kusikiliza na kutatua kero na changamoto za Wananchi wa Mkoa huo Jimbo kwa Jimbo ikiwa ni Mpango wake wa kupatia ufumbuzi kero za Wananchi.
RC Makalla amesema ziara hiyo itaanza rasmi Jumatatu ya August 30 kwenye Jimbo la Kawe Viwanja vya Tanganyika Packers, August 31 Jimbo la Kibamba, September 01 Jimbo la Segerea, Septeā¦