Home LOCAL RC MAKALLA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA LINDI.

RC MAKALLA AKABIDHI MWENGE WA UHURU KWA MKOA WA LINDI.

Na: James Lyatuu, DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo August 23 amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkoa wa Lindi baada ya mwenge huo kukamilisha zoezi la uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi* kwenye miradi ya maendeleo iliyogharimu Zaidi ya Shilingi Bilioni 105.

Zoezi la kukabidhi mwege huo limefanyika mapema Leo mkoani Lindi, ambapo *RC Makalla amesema zoezi la Ukimbizaji wa mwenge mkoani humo limekuwa na mafanikio makubwa.

Aidha RC Makalla amesema licha ya mafanikio hayo miradi mitano Kati ya 46 imeshindwa kupitishwa na Viongozi wa Mbio za mwenge Kutokana na kugubikwa na changamoto mbalimbali.

Kutokana na changamoto hiyo RC Makalla ameahidi kufuatilia kwa kina miradi hiyo na kuhakikisha kila dosari zilizojitokeza zinafanyiwa kazi.

Itakumbukwa mwenge wa uhuru ulikabidhiwa kwa Mkoa wa Dar es salaam August 18 ukitokea Mkoa wa Pwani na kuhitimisha mbio zake August 22 na hatimae leo RC Makalla ameukabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Rajab kwaajili ya kukimbizwa mkoani humo.

Previous articleTCU YAFUNGUA AWAMU YA PILI YA UDAHILI 2021/2022, YAONYA WANAFUNZI KUTOTUMIA VISHOKA.
Next articleKADA WA CCM AHAMAAISHA WANANCHI KUPIGA CHANJO YA UVIKO-19

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here