Home BUSINESS PROFESA MKUMBO BUNGE LIKIRIDHIA MKATABA WA BIASHARA HURU AFRIKA ITASAIDIA KULETA...

PROFESA MKUMBO BUNGE LIKIRIDHIA MKATABA WA BIASHARA HURU AFRIKA ITASAIDIA KULETA USHINDANI.

Kulia ni Waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo akiongea na waandishi wa katika kiwanda cha A to Z, kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti Daniel Baran ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Babati vijijini.

kamati ya Bunge ya bajeti ikielezewa jambo baada ya kufanya ziara katika kiwanda cha A to Z mkoani Arusha.

Watafiti wa kiwanda cha A to Z wakielezea namna wanavyofanya utafiti wa mifuko ya kuhifadhia mazao na vyandarua kabla ya kuingia katika uzalishaji ili kuhakikisha bidhaa wanazozizalisha zinakidhi viwango vya kimataifa

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA

Waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo amesema kuwa wizara hiyo ina mpango wa  kuomba Bunge liridhie Tanzania kujiunga na mkataba wa biashara huru  wa Afrika kwani viwanda  vinahitaji ushindani mkubwa ndani ya Afrika  na Dunia kwa ujumla.

Profesa  Mkumbo aliyasema hayo wakati akiongea na kamati ya Bunge ya bajeti walipotembelea kiwanda cha A to Z katika ziara yao mkoani Arusha ambapo alisema kuwa Tanzania ikisaini mkataba huo itasaidia kufungua masoko katika nchi 54 za Afrika.

“Tanzania imejiunga na jumuiya mbalimbali za kiuchumi EAC na SADIC ambapo kwa kusain mkataba huo itasaidia viwanda vyetu kujipanga zaidi katika kushindana na kiwanda hiki pamoja na vingine uzalishaji wao ni wa kimataifa na bidhaa zinakidhi viwango vya kimataifa,”Alisema  Profesa Mkumbo.

Aidha  Profesa Mkumbo alisema kuhusiana na kamati ya Bunge ya bajeti  mojawapo ya mambo watakaosaidia Ni pamoja na mambo ya kodi ambapo watasaidia kujenga hoja kuishauri wizara ya fedha kuona kwamba  Kodi wanazoziweka  ziwe Ni Kodi ambazo zinachochea uzalishaji katika viwanda pamoja na kuweza kushindana katika soko la ndani ya nchi na ukanda wa Afrika.

Kwa upande wake meneja masoko ya nje kutoka kiwanda Cha A to Z Silvester Kazi alisema kuwa changamoto kubwa zaidi inayokabili ni marejesho ya VAT ambayo yamechelewa sana ambapo wameiomba kamati iweze kusaidia fedha hizo ziweze kutoka kwa wakati ili waweze kuwekeza na kuongeza uzalishaji zaidi.

Alisema kuwa changamoto nyingine ni ongezeko la kodi kwenye nyuzi za pamba kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 25 ambapo wameiomba serikali kurudisha kwenye kiwango cha awali kwani kuna mikataba ya mauzo ambayo walishaingia na haiwezekani kuongeza Bei ya bidhaa hizo tena, hali inayohatarisha ustawi wa kiwanda kutokana na kutarajia kupata hasara.

Naye mwenyekiti wa kamati ya Bunge  ya bajeti Daniel Baran alisema kuwa wamesikia changamoto hizo na Kama kamati wamezichukua ili kwenda kushirikiana na serikali kuutafuta ufumbuzi kwani kiwanda hicho Ni moja kati ya viwanda vinavyofanya vizuri katika ulipaji wa kodi ambapo kwa mwaka wanalipa zaidi ya bilioni 17.

Alisema pamoja na ulipaji wa kodi pia kiwanda kimeajiri zaidi ya watanzania 800 hivyo kamati imejione uhalisia wa bidhaa wanazozizalisha ambapo wameelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuwaandikia changamoto hizo rasmi ili waweze kuzichambua na kuona katika bajeti ijayo Ni namna gani serikali itaingilia kati na kubadilisha viwango hivyo vya kodi.

Previous articleRAIS DK. MWINYI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMISAA WA SENSA YA WATU NA MAKAZI TANZANIA IKULU, ZANZIBAR, LEO
Next articleDITOPILE AWAVAA WANASIASA NA VIONGOZI WA DINI WANAOPOTOSHA KUHUSU CHANJO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here