Home ENTERTAINMENTS NANDY ALAMBA DILI, BILINAS ANAPENDA WATOTO

NANDY ALAMBA DILI, BILINAS ANAPENDA WATOTO

 

NA: MWANDISHI WETU.
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya Faustine Mfinanga ‘Nandy’, ameshukuru wadau wa muziki nchin, kwa kumshika mkono Hadi kupata dili kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Giness Pwani Afrika amesema  mafanikio yake yanachangiwa na upendo wa wadau wa muziki

“Nashukuru uongozi wa Giness, kwa kunipatia ubalozi katika Pwani  ya Afrika naahidi kufanya kazi yangu kwa ufasaha, kikubwaa nawashukuru wadau wa muziki wangu kwa kunishika mkono ndio maana Leo hii thamani yangu inazidi kukua,” anasema Nandy.

Kwa upande wa pili Nandy aligusia picha ya mtoto ambayo aliweka mpenzi wake Bilinasi katika mtandao wa Istagram na kusema kuwa anahisi picha hiyo ni  ya mtoto wake.

“Bilinasi anapenda watoto nahisi ile picha itakuwa ya mtoto wake japo yeye mwenyewe haja niambia zaidi ya kufaham anahitaaji mtoto.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here