Home BUSINESS NAIBU WAZIRI OLE NASHA AFUNGUA KONGAMANO LA KAIZEN BARANI AFRIKA JIJINI DAR.

NAIBU WAZIRI OLE NASHA AFUNGUA KONGAMANO LA KAIZEN BARANI AFRIKA JIJINI DAR.

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Willium Tate Ole Nasha akizungumza wakati akifungua Kongamano la KAIZEN Barani Afrika kwa mwaka 2021 (AKAC2021) lililofanyiaka leo Agosti 24 katika Hoteli ya HYATT REGENCY, Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) mara baada kumalizika kwa zoezi la mgeni rasmi kupita kwenye Mabanda ya wadau wanaotekeleza Falsafa ya KAIZEN waliohudhuria Mkutano huo. PICHA NA: HUGHES DUGILO)


Meneja wa KAIZEN kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bi. Janne Lyatuu akizungumza na waandishi wa habari juu ya Mkutano. PICHA NA: HUGHES DUGILO).

Afisa wa TAN TRADE Samira Mohamed (kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Progamu na Maendeleo ya wafanyabiahara wadogo kutoka TPSF Damas Mugashe (Kushoto) wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mgeni rasmi Naibu waziri (UWEKEZAJI) Mhe. Willium Tate Ole Nasha katika Mkutano huo Jijini Dar es Salaam. PICHA NA: HUGHES DUGILO).

 Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Serikali imesema kuwa kupitia Wizara za Viwanda na Biashara; Fedha na Mipango na Afya, pamoja na Taasisi zilizoko chini ya Wizara hizo wameamua kuunda mifumo ya kuendeleza falsafa ya KAIZEN nchini ili kuhakikisha kuwa falsafa hiyo inaoanishwa kwenye Sera mbalimbali za nchi sambamba ili iweze kusaidia jitihada za Serikali za maendeleo.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (UWEKEZAJI) Willium Tate Ole Nasha wakatiakifungua Kongamano la KAIZEN Barani Afrika kwa mwaka 2021 (AKAC2021) lililofanyiaka  leo Agosti 24 kwa njia ya mtandao katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam lililokutanisha Mataifa zaidi ya 20 yanayotekeleza falsafa hiyo.

Mhe. Ole Nasha amesema kuwa Serikali inatambua jukumu lake la kuboresha mazingira bora ya kufanya biashara ndani na nje ya nchi na uwekezaji ili kuifanya nchi kuwa ya ushindani zaidi katika uzalishaji na shughuli nyinginezo za kiuchumi nakwamba Serikali inaendelea kutoa miongozo na sera mbalimbali na kusimamia utekelezaji wake kwa kila sekta ikiwemo kutoa dira ya namna ambayo kila mhusika atakavyowajibika katika kukabiliana na mapungufu yaliyoko katika eneo lake ili kutatua kero za wananchi.

“Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi inaendeleza sekta ya viwanda kulingana na hali halisi ya soko la Dunia na malengo ya mipango mipana ya maendeleo ya nchi yetu”

“kuanzia mwaka 2007 katika sekta tofauti tumeanza kuitekeleza hii falsafa tumeboesha huduma, tumeongeza mapato kwa kuboresha huduma na namna ya kufanyakazi yote hii imefanywa ili kuongeza ufanisi, kupata huduma bora na kuokoa muda kwa hiyo msingi wa  falsafa ya KAIZEN ni kuona namna gani unavyoweza kujipanga katika mambo haya na hiyo ndio KAIZEN” amesema Mhe. Ole Nasha.

Aidha amesema kuwa kama Serikali inakumbatia farsafa ya KAIZEN kwa sababu inaenda sambamba na mtizamo wao wa namna ya kujenga Taifa la Viwanda, lenye uchumi unaoweza kushindana, pia Taifa lenye uwajibikaji Taifa linaloweza kushindana kiuchumi na nchi nyingine nakwamba wanaamini kila mtu akipata farsafa ya KAIZEN atatimiza wajibu wake wa kuhakikisha anajipanga kutekeleza majukumu yake.

“Sisi kama Serikali tunajipanga tunahimiza hayo yote kwa watanzania tunataka wizara na idara zetu zihakikishe kwamba zinafuata farsafa ya KAIZEN kwa sababu tunahitaji tija tunahitaji kukata gharama tunahitaji uwajibikaji tunahitaji kuwajibika ndio maana leo hii tumefarijika kuandaa mkutano kama huu na Mhe. Rais Samia anafahamu farsafa hii” ameongeza Mhe. Ole Nasha.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jokate Mwegelo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke amesema kuwa falsafa za kijapani zimekuwa zikisaidia sana kuratibu masuala mbalimbali lakini pia kuongeza ufanisi na kwamba makongamano kama hayo yanawapa fursa na viongozi kuweza kujifunza namna ambavyo falsafa hizo kuweza kuwasaidia wananchi.

“Sisi kwenye halmashauri zetu shughuli kubwa ya wananchi wetu ni biashara sasa tunatoa hela nyingi kwa makundi ya kinamama vijana, na makundi mamalumu, sasa tuangalie jinsi gani farsafa hizi zinaweza kuwasaidia wananchi wetu kuweza kufikia malendo yao ya kibiashara” Amesema DC Jokate.

Nakuongeza kuwa “natamani sana mfike kwenye manispaa zetu ili tushirikiane kuwajengea uwezo wa namna gani ya kufikia malengo yao hasa kupitia farsafa hizi na hasa makundi haya ambayo yamekuwa yakijishughulisha na biashara zao kwa kuwezeshwa na manispa zetu kupitia ile mikopo ya halmashauri” Amaeongea Jokate.

 

 

 
Previous articleRC ROSEMARY AWAAPISHA WAJUMBE WA BARARA LA NYUMBA NA ARDHI WILAYA YA MBOWE.
Next articleRC MAKALLA: COCO BEACH KUBORESHWA, KUWA SEHEMU NZURI YA MAPUMZIKO, BURUDANI NA UTALII.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here