Home LOCAL MFUMO WA USAJIRI BASATA WA KIDIGITALI KUANZA HIVI PUNDE

MFUMO WA USAJIRI BASATA WA KIDIGITALI KUANZA HIVI PUNDE

 

 

Na:Adeladius Makwega,WHUSM –Dodoma.

Serikali imesema kuwa kutokana na kuwepo kwa ugonjwa wa Korona Wasanii wanaojisajiriwa na BASATA sasa watatumia mfumo wa Kidigitali badala ya kufika moja kwenye taasisi hiyo ili kupunguza kuenea kwa maambukizi ya Korani nchini.

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mheshimiwa Innocent Bashungwa leo hii wakati alipozikutanisha taasisi kadhaa za wizara hii ambapo pia alitoa maelekezo yake kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo.

“Nimeelekeza huu mfumo wa usajiri uwe vizuri na uwe unafanya kazi kwa haraka, hakuna sababu ya msanii kuja hapa kwani mfumo huu unarahisisha maisha, kama msanii yupo mikoani halazimiki kuja hapa na maisha yanaendelea.” Alisema Mheshimiwa Bashungwa.

Aliongeza kuwa kuna malalamiko kuwa COSOTA, BODI YA FILAMU na BASATA zinafanya kazi kipolisi hili pia limefanyiwa kazi lakini kubwa ni kulinda maadili ya Kitanzania.

“Lazima sanaa iweze kuendeshwa vizuri na siyo jukumu la serikali kudunisha sanaa. Kutakuwepo na mwongozi ya kuyasimamia maadili hayo ili kupunguza malalamiko.” Alibainisha Mheshimiwa Bashungwa.

Nimeiagiza COSOTA kujadili juu ya kanuni itayayozitaka televisheni na redio zote nchini ili kuweza kupata mrahaba wa msanii bila ya kuwa na madhara katika kuendesha vituo cha televisheni na redio

“Namna ya kulipa mrahaba huo nimeagiza tena COSOTA kurudi kwa wadau ili mimi kama waziri mwenye dhamana niweze kusaini kanuni hizo, kwa hiyo natoa wiki moja hii zoezi hilo liweze kukamiliki na wasanii waweze kupata haki zao.” Alisema Mheshimiwa Bashungwa.

Utaratibu huu utakuwa shirikishio kabisa na bila kuathili biashara ya vyombo hivi najua wapo wadau wengine wanaotumia kazi za Sanaa kwa mafano mabasi yanapopiga miziki au kuonesha filamu utakuwepo mfumo mwingine wa ukusanyaji fedha hizo.

Ameongeza kuwa amekutana na kamati ya haki za wasanii ambayo imeundwa ndani ya wizara ili kuyatatua malalamiko yoyote ili yasifike mahakamani.

“Nitaiboresha na kuipa nguvu zaidi kamati hii ni kupunguza kuibuka kawa migogoro ambayo haina ulazima wowote ule.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here