Home BUSINESS KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAFANYA ZIARA TAHA YAAHIDI KUISHAURI SERIKALI UTATUZI...

KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAFANYA ZIARA TAHA YAAHIDI KUISHAURI SERIKALI UTATUZI WA CHANGAMOTO SEKTA YA HORTICULTURE.

Kamati ya Bunge ya bajeti ikielezewa juu ya uzalishaji wa mbegu katika green house katika kampuni ya Rijiczwan iliyopo wilayani Arumeru.
(Kulia) ni  mwenyek wa kamati ya Bunge ya bajeti. Daniel Baran ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Babati vijijini akisikiliza jambo katika ziara yao waliyoifanya TAHA na kushoto Ni mkuu wa wilaya ya Arumeru mhandisi Richard Ruyango.
Mkurugenzi Mtendaji  wa TAHA Dkt Jacqueline Mkindi akielezea maendeleo ya sekta ya horticulture kwa kamati ya Bunge ya bajeti walipoitembelea tasisi hiyo.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Kamati ya Bunge ya bajeti imetembelea Taasisi kilele inayojishughulisha na kilimo cha horticulture (TAHA) na kujionea wanachokifanya pamoja na kujua changamoto zinazowakabili katika kupeleka Sekta hiyo mbele.

Akiongea mara baada ya ziara hiyo mwenyekiti wa kamati hiyo Daniel Baran ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Babati vijijini  alisema kuwa wataendelea kushirikiana na Taasisi hiyo kwani wameona uzito wa jambo wanaokifanya lakini pia wataishauri Serikali vizuri kuhusiana na changamoto zinazowakabili ikiwemo ya ufufuaji wa mashamba ya maua 8 yaliyokufa mkoani Arusha.

Baran alisema kuwa kama kamati wamejionea hali halisi na watapitia changamoto zote na kupeleka mapendekezo kwa serikali kwani sekta hiyo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa nchi na watanzania zaidi ya asilimia kumi wanapata ajira kutokana na kilimo.

Akielezea maendeleo ya Sekta hiyo Mkurugenzi Mtendaji TAHA Dkt Jacqueline Mkindi alisema kuwa wanafanya kazi na vyama vya wakulima 1623 na wakulima zaidi ya elfu 40 ambapo kazi zao ni pamoja na kuangalia mazingira wezeshi, kuongeza tija katika uzalishaji pamoja na ufikiaji wa masoko.

Dkt Mkindi alisema kuwa katika  suala la masoko wapo kwenye mchakato wa kufungua masoko katika nchi ya South Africa, China na India ambapo kuna soko kubwa la mazao hayo na wanahitaji lakini bado nchi ya Tanzania haijaingia mikataba ya masoko na nchi hizo.

Alisema kuhusu usafirisha alisema hadi sasa wanatumia  ndege ya Ethiopia airlines kwaajili ya kusafirisha mazao hayo lakini pia wameanza kutumia bandari za ndani  ikiwemo bandari ya Dar es salaam.

Alifafanua kuwa  sekta hiyo inakuwa kwa kasi ambapo ilikuwa inakua kwa asilimia 11 kwa mwaka lakini kutokana na janga la UVIKO-19 imeshuka na kufikia asilimia 7 pamoja na maeneo mengine ambayo hayafanyi vizuri Kama kufa kwa mashamba ya maua.

Aidha  ameiomba kamati hiyo kusaidia kuishauri serikali kufuta madeni ambayo mashamba yaliyokufa yanadaiwa na kuweza kuwapa wawekezaji wapya nafasi ya kuwekeza kwani mashamba hayo yalikuwa yanaingiza fedha nyingi pamoja na kutoa ajira kwa watanzania.

Pia aliiomba kamati ya bunge ya bajeti kusaidia katika kuhamasisha wananchi kulima mazao ya horticulture hasa ambayo kwasasa yana soko kubwa duniani ikiwemo Pilipili, Parachichi, Nanasi na Embe pamoja na mazao megine ya mboga, mazao ya mizizi, viungo na maua ambayo bado yanafanya vizuri katika masoko ya kikanda na kimataifa .

Naye Mkuu wa Wilaya ya Arumeru  mhandisi Richard Ruyango alisema kuwa ana kero ya wafanyakazi wapatao mia tano na tatu  ambao wanaodai stahiki zao kutoka shamba la Kili Flora lililokufa na wanaodai Billioni 3 na milioni 198.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here