Home Uncategorized KADA WA CCM AHAMAAISHA WANANCHI KUPIGA CHANJO YA UVIKO-19

KADA WA CCM AHAMAAISHA WANANCHI KUPIGA CHANJO YA UVIKO-19

 DAR ES SALAAM.

KADA wa Chama cha Mapinduzi (CCM)kutoka Mkoa wa Dar es Salaam Marijan Murshid amewataka watanzania kuendelea kujitokeza kupata chanjo ili kujilinda na ugonjwa wa Uviko-19 unaoendelea kuisumbua dunia

Aidha amewataka kuachana na malumbano yanayoendelea mitandaoni hususani kwa wale wanaoipinga chanjo hiyo na badala yake wajikite kuhamasishana kupata chanjo hiyo ili pamoja na mambo mengine waweze kuwa salama dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo.

Akizungumza Dar es Salaam Murshid ambaye alikuwa miongoni mwa makada wa CCM aliyejitokeza kugombea Ubunge Jimbo la Ubungo ngazi ya chama katika uchagazi uliopita, alisema kuna kila sababu kwa watanzania kupata chanjo hiyo kwa kuwa imethibitishwa na wataalam wa Afya wa hapa nchini kuwa na uwezo wa kumkinga mtu anayechanja kupata maambukizi ya ugonjwa huo wa Uviko-19. 

“Kikubwa tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya janga la UVIKO-19 kwa kujitokeza kwa wingi katika vituo mbalimbali na kupata chanjo, ni muhimu kufanya hivyo kwa kuwa ina faida kubwa kwetu hususani katika kujilinda na janga hili” alisema Murshid.

Alisema tangu kuzinduliwa kwa chanjo hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan, kumekuwa na muitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza kupata chanjo, suala alilodai kuwa ni vizuri likaendelea ili kuliweka Taifa katika mikono salama.

“Rais wetu Samia Suluhu Hassan amekuwa mfano mzuri kwetu baada ya kuwa wa kwanza kwa kujitokeza kutuzindulia chanjo, kwetu hili ni jambo la faraja kubwa na la mfano wa kuufuata”aliongeza Murshid 

Aidha alisisitiza kuwa hakuna haja kwa watanzania kusikiliza watu wanaotoa maneno mbalimbali hususani mitandaoni kuhusiana na chanjo hiyo kwa madai kuwa wengi wao wamejawa na kebehi wakilenga kuwapotosha watu kupata chanjo hiyo.

Alisema ni muhimu kwa kila mwananchi kupata chanjo hiyo kwa kuwa mbali na kumpa uhakika wa kujilinda na ugonjwa huo pia itawawezesha kuepuka kuwaambukiza wengine ugonjwa huo pale anapokuwa ameambukizwa

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here