Home BUSINESS HABARI,TPSF KUANZISHA BARAZA LA UJUZI WA SEKTA BUNIFU

HABARI,TPSF KUANZISHA BARAZA LA UJUZI WA SEKTA BUNIFU

     

Na: Adeladius Makwega,WHUSM–Dodoma.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakishirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi za Tanzania TPSF wamekutana kujadili adhima na umuhimu wa kuanzisha baraza la ujuzi la sekta binafsi nchini.

Majadiliano haya yamefanyika Agosti 4, 2021 katika kikao baina  ya watendaji wa Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo  na TPSF Mtumba Mji wa Kiserikali Jijini Dodoma.

Akizungumzia suala hilo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mfaume Said amesema kuwa kuanzishwa  kwa baraza hilo itakuwa nafasi ya wadau kujadili na kuwasilisha changamoto zao zilizopo katika sekta ya ubunifu na wataweza kuisadia zaidi serikali  kutokana na yale yanayobainika.

“Pia  tutapata uwezo wa kuwa na  takwimu sahihi  juu ya sekta bunifu hapa nchini na tutaweza kupata soko  la  kazi sanaa  iwe  filamu, muziki, uchongaji, uchoraji, usukaji, ubunifu wa michoro na kazi zingine.” Alisema Kaimu Mkurugenzi huyo.

Hii ni fursa kubwa kwetu na kwa taifa letu kwani  tunajiandaa tuwe na makubaliano ya pamoja ya namna tutakavyoifanya kazi hii kwa manufaa ya kila idara iwe ya michezo, utamaduni au Sanaa.

Akizungumza kuhusu majadiliano  hayo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Francis Nanai alisema kuwa hii ni jambo jema kwa kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ni mdau nambari moja lazima mafanikio haya  yatafanikiwa kwa kiwango cha juu .

“Sisi kama TPSF tumepokea fedha kutoka UNESCO kupitia mradi wa BEAR (III) kwa nia moja ya kuhakikisha baraza la ujuzi la sekta bunifu linaazishwa. Ndiyo maana tumepiga hodi wizara yetu kuelimishana juu ya faida yake kwa wizara na pamoja na wadau wenu.” Alisema  Francis Nanai.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here