Home LOCAL DKT. GWAJIMA AAGIZA JENGO LA MAMA NA MTOTO SEKOU-TOURE KUANZA KUTOA HUDUMA...

DKT. GWAJIMA AAGIZA JENGO LA MAMA NA MTOTO SEKOU-TOURE KUANZA KUTOA HUDUMA KABLA YA DISEMBA 25.


Na: WAMJW- Mwanza.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza jengo la huduma za mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou-Toure kukamilika na kuanza kutoa huduma kabla ya Disemba 31, mwaka huu ili wananchi waanze kunufaika.

Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo leo wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya katika na shughuli za Maendeleo ya Jamii katika Mkoa wa Mwanza ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake iliyoanza Mkoa wa Mara.

“Hapa tulipo bajeti ilikuwa ni Bion 10 na kitu, zimeshatoka Bilion 9 bila matatizo kabisa, na sasa zimebaki Bilion 6 ambazo zimepitishwa kwenye Bajeti hii ya Serikali ya awamu ya 6 ya mwaka 2021-2022, na hizo hela zinatakiwa kuanza kutumika ili zitutoe kwenye asilimia 83 twende kwenye asilimia 100 kabla ya kumaliza tarehe 31 Disemba vitoto vile vitavyozaliwa vizaliwe humu ndani” amesema Dkt. Gwajima.

Amesema, mradi huu, ni mradi mzuri sana, ni mradi mkubwa wenye gorofa sita na vitanda 261 kwaajili ya huduma za Afya ya uzazi na mtoto ambazo zinaweza beba huduma za upasuaji mpaka nne kwa wakati mmoja, huku likiwa na chumba maalum kwaajili ya Watoto njiti, na lina miundombinu kwaajili ya huduma ya hewa ya oksijeni.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema kuwa ili kuendelea kuishi kwa afya njema na kushuhudia maendeleo yanayofanywa na Serikali, ni muhimu kwa wananchi kujikinga na maradhi ikiwemo kupata chanjo ya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa Corona, huku akisisitiza kuwa hata katika nchi za Ulaya wengi waliofariki na ugonjwa huo unaoepukika wengi ni waliokataa kuchanja.

“Usipochanja utapata maambukizi ya ugonjwa wa Corona, na kuwa kwenye nafasi kubwa ya kupoteza maisha, kama wanavyokufa kwenye nchi nyingine zote za Ulaya ambao wamekataa kuchanja” amesema Dkt. Gwajima.

Mwisho.

Previous articleKUTOKA MEZA YA MAGAZETI ASUBUHI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 19-2021
Next articleMABADILIKO YA HADHI YA VYETI VYA USAJILI WA JUMUIYA ZISIZO ZA KIDINI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here