Home LOCAL CCM LAPIGA STOP KUCHAPISHWA GAZETI LA UHURU KWA SIKU SABA

CCM LAPIGA STOP KUCHAPISHWA GAZETI LA UHURU KWA SIKU SABA

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akiongozea mbele ya waandishi wa habari (hawamo pichani) katika mkutano wake na waandishi hao katika ukumbi wa mikutano wa Chama hicho uliopo kwenye Ofisi ndogo za Chama hicho Lumumba Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (kulia) akizungumza wakati wa Mkutano huo na kutangaza kusimamishwa kuchapishwa kwa Gazeti la Uhuru lilipo chini ya Chama hicho. (kushoto) ni Katiku wa Itikadi na Uenezi Sahaka hamdu Shaka.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo (katikati) akiwa na Naibu Katibu Mkuu Bara CCM Mndeme (kulia) na Katiku wa Itikadi na Uenezi Sahaka hamdu Shaka wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye Ofisi ndodo za Chama hicho zilizopo Lumumba Dar es Salaam.

 

Katiku wa Itikadi na Uenezi Sahaka hamdu Shaka akizungumza alipokuwa akimkaribisha Katibu Mkuu wa Chama hicho Daniel Chongolo kuzungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.

Wapiga picha na waandishi wa Vyombo mbalimbali vya habari wakiwa kwenye majukumu yao ya kurekodi na kuchukua habari wakati Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akizungumza na waandishi hao. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

DAR ES SALAAM.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) leo Agosti 11,2021 kimeamua kulisimamisha kwa siku saba Gazeti lake la Uhuru baada ya kuandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho“Sina wazo kuwania urais 2025-Samia” katika chapisho toleo namba 24084 la leo jumatano tarehe 11, Agosti, 2021 huku kikimuomba radhi Rais Samia.
 
Akizungumza leo jiijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi( CCM) Daniel Chongolo amesema huo ni upotoshaji mkubwa wa kumlisha maneno Rais Samia, hivyo kwa nafasi yake ameamua kulifungia gazeti hilo kwa kutochapishwa kwa muda wa siku saba kuanzia kesho Agosti 12,2021,  huku Bodi ya Wakurugenzi wa gazeti hilo ikichukua hatua ya kuwasimamisha kazi watumishi watatu pamoja na kuunda Tume ya kuchunguza habari hiyo ya upotoshaji.
 
Viongozi waliosimamishwa kazi na Bodi hiyo ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Publisher Faustine Sungura, Mhariri Mkuu Ramadhan Athuman Mbwaduke pamoja msimamizi wa zamu aliyesimamia gazeti hilo Rashid Zahoro.

“Naomba kuchukua nafasi hii kumuomba radhi Mwenyekiti wa Chama chetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kulishwa maneno ambayo hakuyasema wakati akihojiwa na BBC, …Uhuru ni gazeti letu hatuwezi kulikana maana hakuna anayeweza kumkana mtoto wake, hivyo tunamuomba radhi Rais wetu.

“Kuomba radhi peke haitoshi,hivyo kwanza naipongeza bodi ambayo leo baada ya kutoka kwa habari hii ya upotoshaji ilikutana na kutoa maazimio kadhaa, tunawapongeza kwa hatua ambazo zimechukuliwa kwa kuwasimisha kazi waliohusika na uandaaji wa habari hii,”amesema.

Gazeti hilo ambalo limetoka leo Agosti 11,2021 limepotosha sehemu ya mahojiano aliyofanya Rais Samia na  Shirika la Utangazaji Uingereza( BBC) yaliyofanyika Ikulu Dar es Salaam .Katika habari yake kuu gazeti hilo limeandika ” Sina wazo kuwania urais 2025- Samia”.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here