Home LOCAL CCM ILALA WAPATA PIGO DIWANI WA BUYUNI AFARIKI

CCM ILALA WAPATA PIGO DIWANI WA BUYUNI AFARIKI

NA: HERI SHAABAN.

CHAMA cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kimepata pigo kufuatia Diwani wake wa Kata ya Buyuni Karimu Madenge kufariki dunia .

Kwa mujibu wa Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM ILALA Said Sidde Marehemu Karimu Madenge alifariki Jana asubuhi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana baada kuumwa kwa muda mfupi.

Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es Salaam , Mwenezi wa CCM ILALA Sidde alisema taratibu za Mazishi  ibada fupi Msikiti wa Buyuni  zinatarajia kufanyika Leo Agosti 05/2021 nyumbani kwa marehemu Buyuni 

Sidde alisema marehemu anatarajia kuzikwa kijijini kwao Kibuta Kisarawe Mkoa wa Pwani saa sita mchana.

Sidde alisema taratibu zote zitafanyika nyumbani kwake Buyuni jirani na Ofisi za CCM .

Sidde aliwataka wana CCM wote kushiriki katika msiba huo  mwezao ikiweno kuchukua tahadhari ya kuvaa Barakoa kwa ajili ya kujikinga na COVID.

Mwisho 

Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI AGOSTI 5-2021
Next articleDKT MKINDI: WANAWAKE TUJITOKEZE KUPATA CHANJO YA UVIKO- 19 TUNA MAMBO MENGI YA KUFANYA KWAAJILI YA FAMILIA ,JAMII NA NCHI KWA UJUMLA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here