Home BUSINESS AFISA MADINI KUMBURU ATATUA MGOGORO YA WACHIMBAJI NA KUWAONYA KUTOKUPELEKA KESI MAHAKAMANI

AFISA MADINI KUMBURU ATATUA MGOGORO YA WACHIMBAJI NA KUWAONYA KUTOKUPELEKA KESI MAHAKAMANI

Na: Saimon Mghendi, Mbogwe

AFISA Madini mkazi wa Mkoa mpya wa  Kimadini Mbogwe Uliopo Wilayani Mbogwe, Mkoani Geita Mhandisi Joseph Kumburu, ametatua mgogoro wa muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya wachimbaji wadogo  wawili wa  Mgodi wa Isajabadugu uliopo Kata ya Nyakafulu, Ambao uliwausisha Slyvester Buyamba na Rashid Said waliokuwa wakigombea maduara.

Kumburu Ametatatua Mgogoro huo jana katika kikao chake na wachimbaji kilichofanyika katika ofisi za Mgodi huo na kuwaonya wachimbaji kutokupeleka kesi za madini  Mahakamani na badala yake wazipeleke katika ofisi yake ili zitatuliwe.

Wawili hao wanadaiwa kupelekana katika ngazi ya Mahakama Kwa Nyakati Tofauti Jambo ambalo lilipelekea  afisa madini  huyo kumuamwandikia barua hakimu akitaka kesi za wachimbaji zisifikishwe mahakamani badala yake zitatuliwe na maafisa  wa mamlaka inayohusika.

Hata hivyo Mhandisi Kumburu  alitoa maelekezo kwa mwenyekiti wa mgodi huo Walwa Katemi, akimtaka kuwachukua hatua kali kwa Wakaguzi watakaechukua rushwa kwa wamiliki wa maduara awfukuze kazi mara moja kwani jambo hilo linaweza kusababisha vifo vya watu wanaoingia kuchimba Dhahabu maduarani.

Katika hatua nyingine Mhandisi Kumburu alisema kuwa ili kukomesha utoroshaji wa Madini ya Dhahabu Katika Mgodi huo serikali kwa sasa inajenga Soko la Dhahabu kama kituo kidogo kwaajili ya kukusanya madini yote ya Dhahabu na kwamba hali hiyo itaondoa kisingizio kwa wachimbaji.

Hata Hivyo Mwenyekiti wa mgodi wa Isajabadugu, Walwa Katemi aliwataka wachimbaji hao kufuata maelekezo yaliyotolewa na afisa Madini kuzuia wizi wa mawe ya dhahabu, utoroshaji wa Dhahabu pamoja na wizi wa dhahabu kwenye mialo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here