Home BUSINESS WAZIRI WA VIWANDA PROF. MKUMBO ATEUA WAJUMBE WA BODI YA TANTRADE

WAZIRI WA VIWANDA PROF. MKUMBO ATEUA WAJUMBE WA BODI YA TANTRADE

Waziri wa Viwanda na Biashara Profesa Kitila Mkumbo amewateua wajumbe saba wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Taarifa iliyotolewa leo Julai 12,2021 na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini inasema kuwa Wajumbe hao walioteuliwa kwa kushirikiana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Omar Said Shaaban imeorodhesha majina ya Wajumbe hao ambao ni, Bwa. Ally Sanga Gugu kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Salim Ahmed Suleiman kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda (SMZ), Bi Vumilia Lwoga Zikankuba kutoka Wizara ya Kilimo, Bw. John Marato Sausi kutoka Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Dorice John Mgetta kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA), Bw. Ahmed Suleiman Nassor kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA), na Dkt. Jackline David Mkindi kutoka Taasisi ya Wafanyabiashara wa Mbogamboga na Matunda Tanzania (TAHA).

Uteuzi wa Wajumbe hao unaanza Mara moja.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here