DAR ES SALAAM.
Wizara ya Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari kupitia Shirika la Posta Tanzania limezindua Duka Mtandao, Duka hilo ambalo litawaunganisha Wafanya Biashara na Masoko ya ndani na nje ya nchi lengo kukuza wigo wa biashara kupitia uchumi wa kidigitali. Halfa hiyo imefanyika katika viwanja vya maonesho ya biashara sabasaba Jijini Dar es salaam, Katika halfa hiyo ya uzinduzi Mgeni Rasmi alikuwa Waziri wa Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari huku Mgeni wa Heshima alikuwa Waziri wa Viwanda na Biashara.
Shirika la Posta likiongozwa na Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel kwa kushirikiana na TanTrade waliweza kutia saini ya Ushirikiano wa Uendeshaji wa duka hilo la Mtandao. Shirika la Posta kwasasa lipo kwenye maboresho makubwa ambapo hivi karibu iliweza kutangaza mpango wake wa kuja na mfumo wa huduma ya pamoja ambapo huduma zote za Serikali zitatolewa sehemu moja.
Kwa upande wa Waziri wa Viwanda na Biashara Prof Kitila Mkumbo amempongeza Waziri wa Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile pamoja na Katibu Mkuu wake Dkt Zainab Chaula wanafanya kazi kubwa katika Wizara hiyo. Lakini pia Prof Kitila Mkumbo amepongeza Kaimu Postamasta Mkuu Ndugu Macrice Daniel kwa kazi kubwa anayo ifanya katika shirika hilo.
Waziri wa Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile amesema yakwamba kwasasa wamejipanga na wapo kwenye maboresho makubwa ya Shirika la Posta kwani mpango uliopo ni kulifanya Shirika hilo kuwa kitovu cha biashara kupitia duka la Mtandao. Lakini pia Dkt Faustine alieleza kuwa hivi karibuni wanatarajia kuanzishwa kwa huduma ya pamoja ambapo Taasisi 13 za Serikali zitatoa huduma kupitia Shirika la Posta kwakutumia mfumo wa huduma ya pamoja.
Mwisho Waziri wa Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari, Waziri wa Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Tecknolojia ya Habari pamoja na Wakuu wa Taasisi na wageni waalikwa waliweza kushuhudia utiwaji wa saini ya uendeshaji wa duka la mtandao baina ya Shirika la Posta pamoja na TanTrade.