Home LOCAL WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI MOROCCO KWA ZIARA YA KIKAZI

WAZIRI MKUU AWASILI NCHINI MOROCCO KWA ZIARA YA KIKAZI

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mohamed V uliopo jijini Casablanca nchini Morroco, Julai 12, 2021.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na  Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli alipowasili katika uwanja wa ndege wa Mohammed V uliopo jijini Casablanca nchini Morroco, Julai 12, 2021.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 12, 2021 amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi.

Akiwasili katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano hususani ya kiuchumi kati ya Tanzania na Morocco.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here