Home LOCAL WAZIRI BITEKO ATAKA MGODI KULIPA FEDHA ZA KIJIJI NDANI YA SIKU...

WAZIRI BITEKO ATAKA MGODI KULIPA FEDHA ZA KIJIJI NDANI YA SIKU 60 MARA.

WAZIRI wa Madini, Dotto Biteko mstari (wa kwanza aliyekunja mikono kifuani) akimsikiliza Mkurugenzi wa Cata Gold Mining, Braam Fankawito (Mzungu) alipofanya ziara ya kikazi mgodini hapo jana.

WAZIRI wa Madini nchini, Dotto Biteko akimsikiliza Mkurugenzi wa Mgodi wa MMB, Yury Chernomorchenko wakiwa kwenye ziara ya kikazi mgodini hapo jana.

MWENYEKITI wa halmashauri ya Musoma, Charles Magoma akitia saini mkataba wa makubaliano kati ya Kijiji cha Seka na Mgodi wa MMB ambao pamoja na mambo mengine unautaka mgodi huo kulipa deni la SH mil. 36 ndani ya siku 60


Na: Mwandishi wetu, MARA.

Waziri wa Madini nchini Tanzania, Dotto Biteko ameutaja Mkoa wa Mara kuwa unashika nafasi ya Tatu kwa kuwa na maeneo yenye wingi wa Madini ya Dhahabu.

“Ukitoa Shinyanga inayobebwa na Kahama na Mbeya inayobebwa na Chunya, Mara inashika nafasi ya Tatu nchini kote kwa kuwa na wingi wa dhahabu,” alisema waziri.

Waziri Biteko alikuwa anazungumza na Mkuu wa Mkoa huo, Ally Hapi alipofika mjini Musoma kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku moja kwenye migodi ya MMG na Cata kwenye halmashauri ya Musoma.

Akiwa MMG Gold Limited, Waziri Biteko aliagiza mwekezaji huyo kulipa deni la Sh milioni 36 ndani ya siku 60 vinginevyo shughuli zote za kiwanda hicho zifungwe.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kuwa Magange Mwita, alisema changamoto kubwa baina ya mgodi huo na wananchi ni deni hilo lililoachwa na uongozi wa mgodi uliopita.

“Makubaliano yalikuwa Sh milioni 60 ililipwa kidogo ikabakia Sh milioni 36 ambazo hazikulipwa tangu Mwaka 2018,” alisema Mwita.

Mwanasheria wa Halmashauri hiyo aliagizwa na Waziri Biteko kushirikiana na uongozi wa mgodi huo kuandika mkataba wa makubaliano hayo ya kulipa deni hilo ndani ya miezi miwili, mkataba ambao ulitiwa Saini na pande hizo mbili kwa kushuhudiwa na waziri huyo.

Kwa sasa mgodi huo unamilikiwa kwa ubia na wawekezaji wawili, MMG Polgon.

Akiwa Cata Gold Mining, Waziri Biteko aliutaka uongozi wa mgodi huo kuzingatia Sheria na Kanuni za Madini nchini hususan wanaponunua bidhaa mbalimbali zikiwamo vipuri vya magari na mitambo na wanapotafuta kampuni za kufanya baadhi ya kazi mgodini.

Kauli hiyo ilifuatia maelezo ya Mkurugenzi wa mgodi huo,Braam Fankawito, kwamba baadhi ya bidhaa ikiwamo vipuri wamekuwa wakiviagiza kutoka Afrika Kusini (South Africa) baada ya uzoefu wao kuonesha vinavyopatikana nchini havina ubora wa kuridhisha na bei ni kubwa ikilinganisha na hali inavyokuwa wanapoagiza nje ya nchi.

“Tumieni utaratibu wa kutangaza tenda, mpate wazabuni wa kutosha na mchague mnayeona anawafaa kwa kuzingatia vigezo mnavyotaka, hapa mngepigwa faini ya Sh milioni 50 lakini serikali haitaki hivyo, tunawalea ili mzidi kukua katika uwekezaji,” alisema waziri

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here