Home BUSINESS WANAFUNZI VETA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUWAANZISHIA MAFUNZO YA MIEZI SITA

WANAFUNZI VETA WAMPONGEZA RAIS SAMIA KUWAANZISHIA MAFUNZO YA MIEZI SITA

DAR ES SALAAM.

Mafunzo yanayotolewa na VETA ambayo yanawawezesha vijjana wa Kitanzania kuweza kupata ujuzi wa ufundi Katika nyanja tofauti yameonekana kuwafurahisha wanafunzi wengi wanaosoma kwenye vyuo hivyo na hivyo kufikia hatua ya kuipongeza Serikali kwa hatua thabiti walipofanya Katika kuisaidia jamii hiyo.


Hayo yameelezwa na moja wa wanafunzi wanaopata Mafunzo hayo kwa miezi sita katika Chuo cha Ufundi VETA Kihonda mkoani Morogoro Nyerere Kalage ambapo amempongeza Rais Samia Suluhi Hassan kwa kutambua amesema iwapo atakutana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua thamani ya vijana wa Tanzania kwa kuhakikisha wanakwenda kupata mafunzo hayo kwenye vyuo mbalimbali vya VETA kote Nchini. 


“Hii imekuwa fursa kubwa kwetu na watanzania wengi wamechangia kozi za VETA ambazo Serikali imeamua kutoa mafunzo bure lakini waliojitokeza ni wengi kuliko ambao wamepata lakini ni matumaini yangu Serikali itaangalia namna bora zaidi ya kuhakikisha vijana wengi wanapata nafasi hiyo ambayo Rais ameamua kuitoa kwa ajili yetu vijana,”amesema.


“Nikiwa kama mwanafunzi na katika maonesho haya tumekuja na mashine ambazo zimebuniwa na wanafunzi na nyingine zimebuniwa na walimu ambazo zinatumika kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo.Tunayo mashine ya kusaga karanga ili kupata siagi ya karanga iliyo bora na inayoweza kuuza sehemu yoyote na ikapata soko.Ameongeza.


Ameupongeza  uongozi wa VETA kwa kuhakikisha inawakutanisha wabunifu kutoka mikoa mbalimbali nchini kwani imekuwa sehemu ya wao wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuona kazi za wengine ambavyo zimefanyika na matarajio yake mwakani naye atakuwa katika maonesho hayo na kitu ambacho atakuwa amekubuni mwenyewe.

Mwisho

Previous articleWAZIRI NDUGULILE ATEMBELEA BANDA LA TCRA SABASABA.
Next articleMISS AFRIKA KUFANYIKA TANZANIA KWA MARA YA KWANZA MWEZI NOVEMBA,2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here