Home SPORTS TIMU YA PRISONS YAPATA DILI LA UDHAMINI WA SOKABET

TIMU YA PRISONS YAPATA DILI LA UDHAMINI WA SOKABETNa: MWANDISHI WETU

Klabu ya Tanzania Prisons inayoshiriki ligi kuu Tanzania, imepata udhamini kutoka katika kampuni ya Sokabet inayo endesha michezo ya kubahatisha nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Msemaji wa Sokabet, amesema mkataba wao na Tanzania Prisons umejikita katika kuhakikisha timu inakuwa na hali nzuri kuanzia kwenye usajili, uendeshaji, maradhi pia kufanya kazi pamoja na timu zaidi.

“Leo tumesaini mkataba wa kuwa wadhamini wa kuu wa timu ya Tanzania Prisons kwa msimu wa 2021-2022 katika ligi kuu ya Tanzania Bara, lutokana na udhamini wetu timu hii ita itafanya uboreshaji wa kiwango cha juu katika kikosi chakae ili kufikia malengo ya kufanya vizuri katika msimu ambao dirishaa la usajili limefunguliwa leo.”

Kwa upande wa Tanzania Prisons Mwenyekiti wa klabu Mkwanda Mkwanda, amesema wamefurahi  kuingia mkataba na kampuni ya Sokabet.

“Tunazo changamoto nyingi kama ukosefu wa Vifaa, viwanja vya mazoezi, maradhi na nyingine tutatumia hii nafasi kama fursa na kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuendeleza soka letu, pia tuna waalika na makampuni mengine kuja kuweza timu yetu” anasema Mkeanda

Alipngeza kuwa swala la mpira wa miguu ni jambo lenye kushika maslahi ya watu wengi, hivyo kuingia mkataba na kampuni ya Sokabet ni imani yetu tutafanya vizuri.

“Tutatumia hii nafasi kama fursa na kuhakikisha tunafanya vizuri ili kuendeleza soka letu, pia tuna waalika na makampuni mengine kuja kuweza katika timu yetu.”

Previous articleNAIBU MEYA WA HALMASHAURI YA JIJI KIMJI AMEWATAKA MADIWANI KUIGA MFANO WA DIWANI WA KIPAWA
Next articleRC MAKALLA- MILIONI 62 ZAHITAJIKA KUBORESHA MACHINGA COMPLEX.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here