Home LOCAL TCRA ZASHIRIKI MBIO ZA MWENGE MAALUM 2021 IPAGALA JIJINI DODOMA.

TCRA ZASHIRIKI MBIO ZA MWENGE MAALUM 2021 IPAGALA JIJINI DODOMA.

Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mabel Masasi akiwapa maelezo viongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ulipowasili katika Shule ya Msingi Ipangala ‘B’ iliyopo jijini Dodoma wakati wa mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio hizo isemayo “TEHAMA ni msingi wa wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji”

Afisa Mwandamizi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)Mabel Masasi  akikabidhi kitabu cha Mwongozo wa Huduma kwa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano Tanzania kwa viongozi wa Mbio za Mwenge Maalum 2020/21 ikiwa ni ishara ya TCRA kuunga mkono kauli mbiu ya mbio za mwenge mwaka huu isemayo “TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu; itumike kwa usahihi na uwajibikaji”

Baadhi ya viongozi wakipata huduma za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Wakati Mwenge wa Uhuru ulipokwenda katika Shule ya Msingi ya Ipagala B jijini Dodoma.

Afisa Habari wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Robin Ulikaye akiwapa elimu wanafunzi wa shule ya msingi Ipagala B Wakati TCRA ikiwa katika ushiriki wa kutoa elimu katika mbio za Mwenge wa Uhuru jijini Dodoma

Previous articleHABARI KUU ZILIZOPO MAGAZETI YA LEO ALHAMISI JULAI 29-2021
Next articleMKUTANO WA WATOA HUDUMA ZA MAHUDHUI NA WADAU WENGINE KATIKA KANDA YA KATI YA TCRA, DODOMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here