Home LOCAL TANZANIA NA UMOJA WA ULAYA ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO

TANZANIA NA UMOJA WA ULAYA ZAAHIDI KUIMARISHA USHIRIKIANO

 
Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti yakiendelea

Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti akimuelezea jambo Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen akiongea na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam

Mazungumzo baina ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen yakiendelea
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akimueleza jambo Kaimu Balozi wa China hapa nchini, Mhe. Xu Chen wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiongea na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Na: Mwandishi wetu, Dar.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) zimeahidi kuimarisha ushirikiano kwa maslahi ya pande zote mbili.

Hayo yamesemwa kwenye mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa nchini, Mhe. Manfredo Fanti, uliofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Sokoine ameeleza kuwa Serikali ya Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ambao umepelekea kuzaa matunda yenye manufaa kwa pande zote mbili. Aidha, ameahidi kuendelea kuimarisha uhusiano huo kwa maslahi ya pande zote.

Kwa upande wake, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) hapa Nchini, Mhe. Manfredo Fanti amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Napenda kukuhakikishia kuwa Umoja wa Ulaya utaendelea kushirikiana kwa ukaribu na Tanzania kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananchi wake,” amesema Balozi Fanti.

Katika tukio jingine, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine pia amekutana kwa mazungumzo na Kaimu Balozi wa China hapa Nchini Mhe. Xu Chen katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wawili walijadili masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa uwili (Bilateral Cooperation).


Previous articleBALOZI LIBERATA MULAMULA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI WA PAKISTAN NCHINI
Next articleKMC FC YAVUNJA KAMBI YA WACHEZAJI WAKE RASMI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here