Home BUSINESS TAN TRADE YAENDELEA KUWANOA WAJASIRILI KUPITIA MIKUTAMO YA ANA KWA ANA.

TAN TRADE YAENDELEA KUWANOA WAJASIRILI KUPITIA MIKUTAMO YA ANA KWA ANA.

KAIMU  Meneja wa  uendeleaji wa Bidhaa  Tantrade Masha Hussein akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa ana kwa ana uliokutanisha wafanyabiashara mbalimbali uliofanyika kwa njia ya mtandao kwenye maonesho maonyesho ya 45 ya kimataifa ya sabasaba Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO).
Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wajasiliamali nchini TWCC Mercy Silla (katikati) akizungumza katika mkutano huo alipokuwa akitoa mada ya namna ambavyo Taasisi yake inavyoshirikisha wanawake kwnye masuala ya kibiashara na ushiriki wao kwenye maonesho hayo. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

 

KAIMU  Meneja wa  uendeleaji wa Bidhaa  Tantrade Masha Hussein (kulia) akiwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza kuhudhuria mkutano huo kwa njia ya mtandao uliozungumzia masuala ya mazao yanafaka. (kushoto) ni Deo Shayo Afisa  anaeshughulikia mazao ya nafaka Tan trade. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)
Meneja masoko wa Bodi ya Mazao ya nafaka Tanzania Fred Mbilinyi akizungumzia namna ambavyo Bodi hiyo inavyofa shughuli zake na fursa mbalimbali wanazozitoa kwa wakulima hapa nchini. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)  
 

Baadhi ya wadau waliohudhuria kwenye mkutano huo ambao pia ulifanyika kwa njia ya mtandao kuwapa fursa wadau wengine kuweza kuhudhuria kutoka kwenye maeneo yao. (PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

KAIMU  Meneja wa  uendeleaji wa Bidhaa  Tantrade Masha Hussein amewataka wafanyabishara nchini kujifunza kuhusu uendeshaji wa biashara nakwamba kwa sasa Dunia inakwenda kwa kasi kutokana na teknolojia hivyo lazima wajifunze ili kujua taarifa muhimu za biashara.

Amesema kuwa wao kama Tantrade wapo kwa  ajili  ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara  lakini kitu kubwa ni lazima wakubali kujifunza ili kuweza kuona dunia inakwendaje na kuna nini katika sekta ya hiyo ya bishara.

Meneja Masha ameyasema hayo leo kwenye viwanja vya maonyesho ya 45 ya kimataifa ya sabasaba ambayo yanafanyika katika viwanja vya mwalimu nyerere barabeara ya kilwa wilayani Temeke.

“Ifike mahala sasa wafanyabiashara wetu lazima wakubali kwamba Dunia inakwenda kasi mno na kila kitu kipo kwenye digitali hivyo kuna haja ya kujifunza na nakuona wengine biashara wanafanyaji ili kuweza kuleta tija katika biashara wanazozifanya nasisi kama wasimamizi tupo kwa ajili ya kuwapa elimu na miongozo “amesema Masha.

Kwaupande wake Mwenyekiti wa Chama cha wanawake wajasiliamali nchini TWCC Mercy Silla amesema kuwa ni muhimu kwa wafanyabishara kuhudhulia mikutano ya ana kwa ana ambayo inaandaliwa na mamlaka ya biashara iliyo chini ya wizara ya viwanda Tantrade ili kupata uewelea zaidi kuhusu masoko na mahusiano ya kibiashara,

Ameongeza kuwa zipo changamoto za masoko kwa baadhi ya wafanyabishara kwakutokujua namna ya kupata masoko hivyo kama watapata wasaa wa kuingia kwenye mikutano hiyo watajifunza mambo mengi yanayohusu biashara na fursa zake.

“kimsingi maonyesho hadi kufikia leo yanaakwenda vizuri na kama mnavyoona hapa kumechangamka na kikubwa wanawake wamejitokeza sana katika maionyesho haya jambo ambalo linaleta faraja hususani kwenye sekta ya biashara hapa nchini”amesema Mercy.

Pia ameendelea  kusisitiza kwa kuwataka wanawake kujitahidi kuboresha bidhaa zao hususani kwenye vifungashio ili kuleta ushindani katika eneo hilo la biashara kwakutambua kuwa ushindani ni mkubwa mno ili lazima kujitangaza  kwa kuwa na bidhaa zilizofungashwa vizuri.

 


 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here