Home BUSINESS TAHA YANG’ARA MAONESHO YA SABASABA DAR.

TAHA YANG’ARA MAONESHO YA SABASABA DAR.

Afisa lishe kutoka TAHA Salome Stephen (kushoto) na Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka TAHA Magdalene Mhina (kulia) wakionyesha Mazao ya Sltrucurture.
Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka TAHA Magdalene Mhina akionyesha bidhaa za kilimo zinazozalishwa na wakulima wa Taasisi hiyo.
Afisa ufuatiliaji na Tathimini kutoka TAHA Magdalene Mhina akitoa maelezo kwa mgeni alifika kwenye Banda lao.

Afisa Utawala TAHA Morogoro Philemon Mduma (kulia) akiwahudumia wananchi waliofika kwenye Banda lao kujifunza Mambo mbalimbali ya Taasisi hiyo.

Afisa Uhusiano kwa Wateja wa TAHA  Lovennes Adolf Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.


Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Watanzania hususani Vijana wameshauriwa kufanya kilimo cha Biashara kitakachoweza kuwahakikishia kupata kipato cha uhakika na kuendesha maisha yao.

Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano kwa Wateja wa Shirika hilo  Lovennes Adolf alipozungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimatafa (Sabasaba) ambapo amesema kuwa TAHA wamekuwa jukwaa la kutoa sauti kwa wazalishaji, wafanyabiashara, wauzaji bidhaa pamoja  na wasindikaji wa mazao ya horticulture na kwa kwamba wakulima waliopo chini ya Taasisi hiyo wameweza kunufaika kwa kiasi kikubwa na kilimo hicho.


“Ndugu zangu wanahabari TAHA Tunatekeleza shughuli zetu kupitia mfumo wa kongani kama sehemu ya kufikia jamii ambazo zimelengwa kikamilifu hivi sasa, Amesema Lovennes.


Akizungumzia maonesho hayo  amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maonesho na ushiriki wao  umeweza kusaidia kukutana na wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakifika kutaka kufahamu  shughuli za TAHA.


Amefafanua kuwa  matumaini yao kama TAHA  baada ya kumalizika kwa maonesho hayo watakuwa wamepata mabalozi wazuri ambao watakuwa mstari wa mbele kuitangaza Taasisi hiyo.


“Hii ni  fursa kubwa kwani baada ya maonesho haya tunaamini kila aliyepita hapa atakuwa Ballozi mzuri wa kuitangaza Taasisi yetu. Ameongeza

Previous articleMEYA KUMBILAMOTOK KUZINDUAUPIMAJI AFYA BURE ZAHANATI YA ISMILLA
Next articleMAGAZETI YA LEO J.TANO JULAI 14-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here