Home BUSINESS STAMICO KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO NCHINI

STAMICO KUWASAIDIA WACHIMBAJI WADOGO NCHINI

Na: Cymon Mgendi, SHINYANGA.

Shirika la madini la Taifa STAMICO kupitia mgodi wake wa STAMIGOLD limesema kuwa limejikita katika kutafiti,kuchimba Pamoja na kuchenjua dhahabu na mara baada ya kupata dhahabu wanaziuza kwenye soko la ndani katika kiwanda cha Mwanza Precious Metal kilichoopo jijini Mwanza.

Akifafanua Mbele ya waandishi wa habari katika maonesho yanayoendelea kwenye viwanja vya Zainabu Telack vilivyoopo kwenye kata Old Shinyanga kaika manispaa ya Shinyanga, Afisa  Raslmali watu Bunda Nyakiroto, kutoka mgodi wa STAMIGOLD uliopo Biharamulo, amesema kuwa kampuni hiyo imekua ikiwawezesha wachimbaji wadogo.

“Mgodi wetu uliopo Biharamulo umekua ukisaidia jamii inayo huzunguka mgodi huo kwa kufanya shughuli za kijamii, mbali na ajira kwa wazawa lakini pia mgodi huo umegeuka soko kwani hununua vyakula kwenye vijiji hivyo, kwahiyo wakulima na wafugaji wanapata huakika wa soko”, alifafanua Nyakiroto.

Aidha Afisa huyo alisema kuwa mgodi wake unawapa kipaumbele wazawa kwani mpaka sasa wameajiri Zaidi ya watanzania 230 pamoja na kusaidia mambo mbalimbali katika jamii inayowazunguka ikiwemo kujenga zahanati.

Pia Nyakiroto alitumia fursa hiyo kuwashauri wachimbaji wadogo kujiuga kwenye vikundi ili shirika liweze kuwasaidia kiurahisi tofauti akikaa kila mchimbaji mmoja mmoja.

Previous articleKOCHA WA YANGA NASREDDINE NABI ATWAA TUZO YA KOCHA BORA YA MWEZI JULAI
Next articleRC MKIRIKITI: HALMASHAURI TEKELEZENI MIRADI YA MAENDELEO KWA UBORA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here