Home LOCAL RC MAKALLA: UVAAJI BARAKOA KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI NI LAZIMA.

RC MAKALLA: UVAAJI BARAKOA KWENYE VYOMBO VYA USAFIRI NI LAZIMA.

– Awataka LATRA kusimamia Level seat.

– Aelekeza Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya kusimamia Utekelezaji wa Mwongozo wa Wizara ya Afya.

DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku Wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma pasipo kuvaa barakoa.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo Kufuatia Mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya ambapo amesema watafanya ziara za kustukiza kwenye Vituo vya Daladala, Feri, Stendi, Mabasi ya Mwendokasi, maeneo ya Masoko na sehemu zote za kutoa huduma ili kuangalia Utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha RC Makalla amesema Serikali imejipanga kutoa huduma Bora za matibabu kwa wagonjwa wote watakaofika hospital na kuwataka Wananchi watakaoona dalili za Corona kuwahi vituo vya Afya.

“TUNAKULINDA NA WEWE UTULINDE, VAA BARAKOA KWA MUSTAKABALI WA AFYA YAKO NA WENGINE.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here