Home LOCAL RC MAKALLA AAGIZA MAENEO YA WRONG PARKING YABANDIKWE VIBAO.

RC MAKALLA AAGIZA MAENEO YA WRONG PARKING YABANDIKWE VIBAO.

DAR ES SALAAM.

-Aagiza waliojipa majukumu ya kunyemelea kukusanya Wrong Parking wasakwe Mara moja.

-Ataka TARURA na Wakurugenzi kutoa elimu na kuweka Vibao. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezielekeza Halmashauri kwa kushirikiana na TARURA kuhakikisha wanaweka Vibao vya Wrong Parking kwenye maeneo yasiyo rasmi kwa maegesho ili kuepuka uonevu.

RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao alichohitisha baina yake, Wakurugenzi wa Halmashauri na TARURA kilicholenga kuondoa kero ya tozo ya Wrong Parking.

Aidha RC Makalla amesema kikao hicho wamekubaliana tozo ya Wrong Parking itekelezwe kwa mujibu wa Sheria lakini kwa mtu ambae ataonekana alidhamiria moja kwa moja kuvunja Sheria huku akisisitiza  Elimu iendelee kutolewa.

Pamoja na hayo RC Makalla ameamua kuunda timu ya wataalam kwajili ya kuandaa mfumo mzuri wa Mapato ili kuhakikisha kiasi Cha tozo kinacholipwa kinaenda moja kwa moja serikalini na muhusika anapatiwa risiti ili kuepuka udanganyifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here