Meneja wa mafao mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa serikali(PSSSF) Mkehenge Ramadhani akiongea na waandishi wa habari katika semina yao kwa wastaafu watarajiwa mkoani Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Sophia Mjema akiongea na waandishi wa habari baada ya kufungua semina kwa wastaafu watarajiwa mkoa wa Arusha iliyoandaliwa na PSSSF. |
Meneja mwandamizi wa wa wateja binafsi wa benki ya NMB Ally Ngingite alikieleza jinsi benki hiyo inavyowajali wastaafu. |
Lempere Oloije mstaafu mtarajiwa kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro akielezea umuhimu wa mafunzo hayo |
Na: Namnyak Kivuyo, Arusha.
Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma(PSSSF) imetoa mafunzo kwa watumishi 350 kutoka wilaya zote za mkoa wa Arusha wanatarajiwa kustaafu katika kipindi cha mwaka 2021/2023 ili kuweza kutumia fedha zao vizuri wanapostaafu pamoja kuepuka matapeli.
Akifungua semina hiyo ya siku mbili ya kuwapa elimu ya uwekezaji kwa maisha endelevu baada ya kustaafu mkuu wa wilaya ya Arusha Sophia Mjema alisema kuwa kumekuwepo na tatizo la wastaafu kutapeliwa fedha zao pindi wanapostaafu huku wengine wakitumia fedha hizo bila mpangilio na mahesabu na kuto kujua kuwa wanavyotumia fedha hizo zinaisha.
Mjema aliwataka wastaafu hao kuacha kuangalia familia za watoto wao na kujiendeleza wao binafsi kwani muda wao wakuangalia familia zinazojiendeleza umeisha na uliobaki nikujijali wenyewe na kuangalia namna watakavyotumia fedha hizo hadi pale ambapo watapoteza maisha.
Aidha aliwataka pindi wanapopata fedha hizo wazitumie kwa ajili ya kujenga maendeleo ya nchi na taifa kwa ujumla huku wakijitahidi kujiendeleza kwa kuwekeza katika kilimo biashara ,ufugaji na mambo mengine mengi huku akibanisha kuwa fedha wanazopewa sio nyingi maana aziongezeki bali zinapungua kwa iyo ni vyema wakatumia vyema.
Alisema kuwa ana imani semina hii itasaidia kuwaondolea matatizo ambayo wastaafu wamekuwa nayo moja wapo ikiwa ni matumizi sahihi ya fedha na kuepuka kutapeliwa na pia fedha za wastaifu zitatumika vizuri kuongeza pato la wastaafu.
“Naimani mkitoka hapa hakuna atakayedanganyika tena baada ya semina, zingatieni mkitoka hapa mjue mnaenda kufanya nini ili msiende kubabaishwa wala kuyumbishwa,” Alisema.
Kwa upande wake meneja wa mafao mfuko wa hifadhi ya jamii (PSSSF) Mkehenge Ramadhani alisema kuwa mfuko wao umeanza kutoa mafunzo hayo baada ya kuona matatizo mengi ambayo wastaafu wanakutana nayo hasa ya kutapeliwa nakutumia vibaya fedha zao baada ya kustaafu jambo ambalo linawafanya kuanza kuangaika baada ya muda mfupi wa kustaafu.
Alisema waliona ni vyema wakawapa mafunzo kwaajili ya kuwaandaa kwa maisha ya baadaye ambapo zoezi hilo lilifunguliwa rasmi mkoani Dodoma na linatarajiwakufanyika katika mikoa yote hapa nchini na zaidi ya wastaafu 8000 wanaotarajia kustaafu watapatiwa elimu hiyo kwani zoezi hilo ni endelevu.
Naye meneja mwandamizi wateja binafsi na maalum wakiwemo wastaafu kutoka benki ya NMB ambao ni mmoja kati ya wathamini wa mafunzo hayo Ally Ngingite alisema kuwa benki yao inawajali sana wastaafu na ndio maana wakaanzisha huduma mbalimbali zinazowahusu ikiwemo kuwapa mikopo wastaafu ,upatikanaji wa fedha kirahisi kwa maana ya mitaji pamoja na kuwapa bima ya afya.
“Katika eneo la uwekezaji kwa wastaafu kuna akaunti maalum ambazo hazina makato na zitawezesha wateja wetu wastaafu kujiekea amana na akiba za muda mfupi na mrefu ambazo wataweza kutumia Kama dhamana ya kuchukulia mikopo kwaajili ya mitaji kwahiyo mtaona tumejikita kuhakikisha kwamba wastaafu hawa wanaenda kufurahiya maisha yao katika kujiongezea kipatoka kwenye kilimo, biashara za ujasiriliamali na nyinginezo kwasababu NMB tunaamini kuwa kustaafu sio mwisho wa maisha,” Alisema.
Mmoja wastaafu watarajiwa kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Lempere Oloije alisema kuwa semina hii itawasaidia kupata elimu ambayo itawasaidia kuendelea maisha baada ya kustaafu kwani watajua namna ya kutumia fedha za mafao watakapozipata.