Home BUSINESS MWENGE WA UHURU WAZINDUA KIWANDA KIKUBWA CHA PLASTIC KAHAMA

MWENGE WA UHURU WAZINDUA KIWANDA KIKUBWA CHA PLASTIC KAHAMA

 Na:Saimon Mghendi, KAHAMA

Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa Kiwanda cha KAHAMA PLASTIC INVESTIMENT kilichotumia takribani  Tsh. Bilioni 5 kwa sasa kilichoopo kwenye Kata ya Mhongolo manispaa ya kahama  Mkoani Shinyanga.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi, amesema hatua ya Muekezaji Mzawa, Hamisi Mhoja Bundala kuanzisha kiwanda cha KAHAMA PLASTIC INVESTIMENT  kumesaidia wananchi wengi kupata ajira.

Luteni Josephine Mwambashi ameyasema hayo leo alipokua akizindua mradi wa kiwanda hicho na kuongeza kuwa Kiwanda hicho kinafaida kubwa kwa wakazi wa eneo hilo Pamoja na Taifa kwa ujumla.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, amesema kuwa awali mtu alipokua akiokota mifuko chakavu pamoja na plastiki alikua akionekana kichaa, lakini kwa sasa imekua ni ajira kwa sababu uchafu huo umegeuka kuwa malighafi ya kiwanda.

Awali akitoa taarifa fupi mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kiataifa Meneja mkuu wa kiwanda hicho Desidely Magili, amesema kuwa mradi wa kiwanda hicho umetumia takribani Tsh. Bilioni 5 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka 2026 na utakua umetumia Tsh. Bilioni 8

Kwa upande wake Muekezaji Mzawa wa Kiwanda hicho Hamisi Mhoja Bundala ameishukuru serekali ya awamu ya sita kwa kutambua na kuthamini mchango wa wawekezaji wazawa na kutumia fursa hiyo kuiomba serekali iweze kuboresha mazingira ya mikopo kupitia benki ili wawekezaji wengine  waweze kukopa kwa uraisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here