Mjasiriamali anaejishughulisha na utengenezaji wa Bidhaa za mikono Sarah Lutahya ameipongeza Serikali kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuandaa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yaliyokuwa na ufanisi mkubwa.
Sarah ambae pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Byera Fashion Tz amesema kuwa Maonesho hayo yaliyoanza Juni 28,2021 na kufunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. Philip Mpango Julai 5,2021 yalianza vizuri huku watu wakiongezeka kila siku nakwamba yalileta fursa kwao kama wajasiriamali kuweza kufahamiana wao kwa wao na kutengeneza mtandao wa kibiashara huku wananchi mbalimbali waliojitokeza wakipata fursa ya kununua bidhaa zao.
Mjasiriamali huyo mwenye uzoefu mkubwa katika fani ya ubunifu wa kazi za mikono na ushonaji wa mavazi ya Kiafrika ameweza kushiriki maonesho hayo kwa miaka kadhaa hivyo yamekuwa yakimjenga kila wakati na kumfanya kukua kibiashara.
Kampuni hiyo yenye makazi yake Jijini Dar es Salaam inajishughulisha na utengenezaji wa Bidhaa mbalimbali za Mikono zikiwemo mabegi ya aina tofauti, mikoba ya wanawake, nguo za Asili la Bara la Afika na vitu vingi vya kiasili.
Sarah amewasihi Watanzania wote kwa ujumla kupenda kutumia bidhaa za Asili kwani kwa sasa wajasiriamali wamekuwa wakitengeneza Bidhaa zenye ubora wa juu na kuweza kupata soko nje ya nchi.
Kwa ujumla, kampuni hiyo inatengeneza vitu vyenye mtazamo wa utamaduni wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kwa mawasiliano unaweza kumpigia simu namba +255 784 729416, Barue pepe: sarahlutahya@gmail.com, au unaweza kumtembelea Ofini kwake Masaki mtaa wa Mwaya, kitalu Na: 1549.