Afisa Tawala Zahanati ya Isimila |
NA: HERI SHAABAN.
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto anatarajia Kuzindua upima Afya Bure siku ya Alhamisi Julai 15/2021 pamoja na uzinduzi wa zahanati ya ISIMILLA wilayani Ilala.
Upimaji huo wa afya bure sambamba na kuzindua zahanati hiyo unatarajia kuanza saa mbili asubuhi hadi jioni katika zahanati ya ISIMILLA wilaya ya Ilala.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Afisa Utawala wa Zahanati wa ya ISIMILLA Lordriguez Peter alisema Meya Omary Kumbilamoto atazindua upimaji wa afya bure katika zahanati hiyo huduma zitakazotolewa bure ushauri Nasaha ,kupima Kisukari ,wingi wa damu ,presha na uchangiaji wa damu pamoja na kupima magonjwa nyemelezi.
Afisa Utawala Peter alisema kituo chao cha kisasa kina madaktari bingwa wa Mama na Mtoto na Wataalam katika kada ya afya amewataka wananchi wa Wiĺaya ya Ilala na Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza siku hiyo kupata huduma bora.
“Zanahati yetu ya ISIMILLA ina madaktari wa kisasa wakiwemo madaktari wa watoto na daktari wa Wanawake inatoa huhuma kwa magonjwa yote katika zahanati yetu ikiwemo vipimo vya Mahabara na Bima ya Afya (NHIF ) ” alisema Peter.
Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupima afya bure kwa ajili ya upimaji wa magonjwa mbalimbali kwani kuangalia afya mapema ni bora zaidi kuliko kutibu ugonjwa.
Mwisho