Home SPORTS MBUNGE BONAH KUZINDUA DIWANI CUP KIPAWA

MBUNGE BONAH KUZINDUA DIWANI CUP KIPAWA

Picha Na: Maktaba.

NA: HERI SHAABAN.

MBUNGE wa Jimbo la Segerea BONAH LADISLAU KAMOLI anatarajia kuzindua mashindano ya Diwani Cup Kata ya kipawa Julai 17/2021

Mashindano hayo ya Diwani Cup Kipawa yameandaliwa na Diwani wa Kata Aidani Kwezi ambapo yameshirikisha timu 32 na timu nane za wanawake 

 .Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mratibu wa mashindano hayo Aidan Mkwezi alisema katika mashindao hayo mshindi wa kwanza Ngombe na mshindi wa pilï anatarajia kuondoka na mbuzi.

“Michezo ni afya michezo ajira pia inajenga udugu tumeandaa mashindano haya ya diwani cup kipawa kwa ajili ya kuwashirikisha wananchi kujenga mausihano na jamii kuacha kushiriki katika vitendo viovu” alisema Aidan.

Diwani Aidan alisema  mashindano hayo yatakuwa na hatua ya mtoano na timu zitakazo ingia fainaili watapata zeji seti moja  mfungaji bora atazawadiwa viatu na mpira ambapo golikipa bora atapewa gloves .

Alisema michezo hiyo ya Diwani Cup kipawa itakuwa ikitangazwa na kituo cha radio Times Fm 100.5

Aliwataja wageni walikwa wengine Meya wa halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto,Naibu Meya Saidy Kimji na Afisa Maendeleo wa halmashauri ya Jiji wa Dar es Salaam Fransica Makoye.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here