Home LOCAL MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MKURUGENZI WA AFD (PICHA)

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA NAIBU MKURUGENZI WA AFD (PICHA)

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Ufaransa (AFD) Bi. Marie-Hellen Loison. Mazungumzo hayo yamefanyika Paris Nchini Ufaransa
Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango akimkabidhi zawadi ya mchoro wa Mlima Kilimanjaro  Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Maendeleo ya Ufaransa (AFD) Bi. Marie-Hellen Loison mara baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao Paris –  Ufaransa.

Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amekutana na kufanya  mazungumzo na Bi. Marie-Hellen Loison, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa, hii leo  2 Julai 2021 Pris Nchini Ufaransa. Mazungumzo baina ya pande mbili yalijikita kujadili masuala mbalimbali ya kukuza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Shirika hilo

Mheshimiwa Makamu wa Rais amelishukuru shirika hilo na Serikali ya Ufaransa kwa ujumla kwa kuendelea kutoa ufadhili kwa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika sekta ya maji, usafi wa mazingira, nishati, elimu na utalii.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu huyo, ameeleza  kuwa shirika hilo limepandisha hadhi ya ofisi yake jijini Dar es Salam kuwa ofisi ya kudumu tangu mwaka 2018 na lipo kwenye mchakato wa kufungua Ofisi ndogo jijini Dodoma ili kuwa karibu na Wizara/Taasisi mbalimbali za Serikali ambazo inashirikiana nazo.

Bi Marie Hellen amesema shirika hilo limedhamiria kupanua wigo wa ushirikiano wake na Tanzania ikiwa ni pamoja na kuibua maeneo mapya ya kuendeleza ushirikiano. Aidha amesema tayari wameweka nia ya kuwekeza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hasa katika masuala ya uchumi wa Buluu, Utunzanji wa mazingira,kilimo  pamoja na kutilia mkazo masuala ya kijinsiausawa wa ni;

Akichangia hoja hiyo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alilishukuru shirika hilo kwa kuchagua maeneo muhimu ambayo yanagusa maisha ya wananchi wa kawaida moja kwa moja. Alimfahamisha Naibu Mkurugenzi Mkuu kuwa maeneo hayo pia ni vipaumbele vya Serikali ambayo yameainishwa katika Mpango wa Tatu wa Maendeleo uliozinduliwa hivi karibuni. Sambamba na maeneo hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais aliainisha sekta ambazo zimeendelea kuwa za kipaumbele ikiwa ni pamoja na miundombinu, nishati, kuboresha miundombinu ya maji ambazo zitasaidia kuchochea Tanzania ya Viwanda ambayo ilikuwa moja ya malengo ya Mpango wa Pili wa Maendeleo (FYDP II). Aidha, kutokana na umuhimu wa shirika hilo kwa Tanzania, Mheshimiwa Makamu wa Rais alimhakikishia ushirikiano wa Serikali ya Awamu ya Sita katika kutekeleza majukumu ya shirika hilo nchini.

Previous articleMHE. RAIS SAMIA AONGOZA KUAGA MWILI WA MHANDISI MFUGALE
Next articleMAGAZETI YA LEO J.MASI JULAI 3-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here