Home LOCAL HISTORIA YA NCHI YETU HAIWEZI KUKAMILIKA BILA YA HAYATI MZEE MKAPA’-RAIS SAMIA

HISTORIA YA NCHI YETU HAIWEZI KUKAMILIKA BILA YA HAYATI MZEE MKAPA’-RAIS SAMIA

 

Na. Georgina Misama- MAELEZO

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Rais Mtaafu wa Awamu ya Tatu Hayati Benjamin Mkapa alikuwa kiongozi wa tofauti kwani alikuwa jasiri, shupavu, imara, mpenda maendeleo, mwanadiplomasia  aliyekuwa na maono makubwa  ya ndani na nje ya Tanzania.

Akizungumza leo, Jijini Dar es samaam katika Kongamano la Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa Hayati  Mkapa, Rais Samia alisema kwamba kitabu cha historia ya Tanzania hakiwezi kukamilika bila kuwepo kwa sura nzima yenye kumwelezea Hayati Mkapa na magezi mengi aliyoyafanya katika uongozi wake.

“Kitabu cha historia ya Taifa letu hakiwezi kukamilka bila kuwepo kwa sura nzima itakayomwelezea Hayati Mzee Mkapa, sio tu kwasababu alikuwa Rais wetu, lakini pia kutokana na mageuzi makubwa aliyoyafanya kwenye nchi yetu. Alikuwa mtu wa kipekee sana, mara zote ukikutana nae utaondoka umechota maarifa mengi”, alisema Rais Samia. 

Aidha, Rais Samia amesema kwamba Hayati Mkapa ndie alienzisha taasisi nyingi nchini ambazo bado zinaendelea kufanya kazi nzuri mpaka leo. Akizitaja baadhi ya Taasisi hizo ni pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania (PCCB) pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF). Taasisi nyingine ni Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKURABITA) na Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS).

Kwa upande wa maendelea ya uchumi wa nchi kwa ujumla Rais Samia alisema kwamba Hayati Mzee Mkapa alifanikiwa kupunguza deni la Taifa kutoka asilimia 143.7 mwaka 1995 hadi asilimia 60.7 mwaka 2005 akichochewa na uwezo wake wa kidiplomasia katika kuzishawishi Taasisi za kifedha za Kimataifa na Nchi wahisani  kusamehe madeni kwa kutumia mpango wa  Heavily Indebted Poor Countries (HIPC) uliosimamiwa na Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Ukiachilia mbali shughuli hizo alizozifanya nchini, Hayati Mzee Mkapa pia alikuwa nguzo hata katika Mataifa mengine ambapo alisimama kidete katika kusuluhisha migogoro baina nchi na nchi kama ule mgogoro wa Burundi, lakini pia alishiriki midaharo ya Kimataifa na kutetea kile alichokiami mafano masuala ya utandawazi alikuwa mstari wa mbele kujipambambanua kwamba Dunia ya sasa ni ya utandawazi.

Kongamano hilo lilijumuisha mdahalo ambao uliwahusisha wanataaluma ngulia wa masuala ya Afya Duniani, akiwemo Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro, mwakilishi wa Mambo ya Afya wa Shirika la Maendeleo la Marekani Balozi Dkt. Donald Wright, Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Bwn. Sanjay Rughani pamoja na Mtaalam Mwandamiazi wa Masuala ya Afya na Jinsia, Dkt. Fatma Mrisho, Rais Samia alisema amefurahishwa na mjadala huo ambao ulilenga kwenye masuala ya Afya.

“Nimefurahishwa sana na mdahalo huo, kwa kuzingatia Serikali ipo kwenye mpango wa kuanzisha Bima ya Afya kwa wote. Wataalamu wetu wa Afya wako hapa, natumai wameyasikia na kuayachukua ili kuyafanyia kazi’.  

Rais Samia ameipongeza Taasisi ya Benjamin Mkapa chini ya uongozi wa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. Ellen Mkondya pamoja na  Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Adeline Kimambo kwa kuandaa kongamano hilo lililoenda sambamba na uzinduzi wa Mfuko wa Wakfu ambapo Rais Samia aliahidi Serikali itachangia mfuko huo. Aidha, Rais  amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuendeleza mambo mazuri yanayoachwa na viongozi wa Kitaifa pindi wanapofariki kama njia ya kuwaenzi na kurithisha vizazi vijavyo tunu ambazo nchi yao imebarikiwa nazo.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here