Home SPORTS CLABU YA YONGWE FC CHANIKA WAANDAA...

CLABU YA YONGWE FC CHANIKA WAANDAA BONANZA

Kocha Mkuu wa Yongwe FC (Abdalah Salehe ((kushoto)akikabidhi cheti cha Usajili kwa Katibu wa Yongwe Rashid Mtimbange Dar es Salaam Jana Klabu ya Yongwe FC imepata usajili wake mwaka huu (PICHA NA HERI SHAABAN)

Wachezaji wa Timu ya Yongwe FC iloyopo Chanika wakigongesha chupa kifurahi usajili wa klabu yao Jana Julai 25/2021)(PICHA. NA HERI SHAABAN).

NA: HERI SHAABAN( ILALA)
CLUB ya Yongwe FC inatarajia kuandaa Bonanza lake Agosti mwaka huu kwa ajili ya kutambulisha klub yao mpya .
Akizungumza na gazeti hili Chanika Wilayani Ilala wakati wa kukabidhi katiba na Cheti cha usajili wa klub hiyo Kocha Mkuu wa timu hiyo Abdalah Salehe Haule ,alisema club ya Yongwe Fc inatarajia kufanya bonanza la kata. tarehe  7  Agosti Dhumuni la bonanza hilo ikiwemo utamburisho wa Timu yao na Club .
“Tumefanikiwa kupata usajili na katiba kwa ajili timu yetu ya Yongwe ambayo inajiandaa katika mashindano mbalimbali ngazi ya Wilaya na mkoa kwa ajili ya kuitangaza kata yetu ya Chanika “ alisema Haule
Haule alisema Yongwe FC kwa sasa ina wachezaji 32 wa timu hiyo na timu ya vijana  ina Wachezaji 19   mpaka sasa.
Aliwataka wachezaji wa klabu hiyo kuwa na nidhamu katika Michezo kwani Michezo ni ajira ,Afya na ujenga mahusiano kwa jamii .
Aidha Haule aliweka wazi  mikataba ya Klabu hiyo   malengo yao mengine kuweka mikataba ya vijana wa michezo watakaojiunga na klabu hiyo  .
Alisema malengo mengine ya klabu ya Yongwe kushiriki ligi mbalimbali ikiwemo daraja la tatu mpaka ligi ngazi ya mkoa.
Aliwataka vijana kushiriki michezo kwani michezo ni ajira washishiriki katika makundi ya vijana wa mitaani wakaingia katika makundi yasio fahaa.
Alisema mikakati yao ya baadae kuanzisha ligi ya Wanawake itakayokuwa inatoa burudani ngazi ya Wilaya na mkoa .
Akielezea changamoto za timu hiyo alieza ukosefu wa jezi za kutosha na mipira kutokana na clabu hiyo bado changa ameomba wadau mbalimbali kuwasaidia kwa ajili  kufikia malengo.
Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here