Home BUSINESS BRELA YANG’ARA MAONESHO YA SABASABA.

BRELA YANG’ARA MAONESHO YA SABASABA.

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa akiwa ameshika kombe la ushindi wa tatu katika kundi la Kuwezesha biashara na Uwekezaji, baada ya kukabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Washiriki wa maonesho ya sabasaba kutoka BRELA wakiwa katika pamoja baada ya kupata cheti cha ushindi wa tatu katika kundi la kuwezasha biashara na uwekezaji.

Picha Mbalimbali za baadhi ya watumishi wa BRELA wakifurahia TUZO waliyopata.
Ofisa Leseni wa BRELA Bi. Rehema Kionaumela (kushoto) akimkabidhi Cheti Moja ya Mwananchi aliyefika kwenye Banda lao na kufanya usajili wa papo hapo wa jina la Biashara na kupata Leseni yake kwenye Maonesho ya Sabasaba yaliyofungwa rasmi julai 13,2021 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Elimu kwa Umma BRELA Roida Andusamile (kush0t0) akitoa Elimu kwa Mwananchi aliyefika kwenye Maonesho hayo kufahamu huduma mbalimbali za Taasisi hiyo.
Afisa TEHAMA wa BRELA Hillary Mwenda (kulia) akimhudumia Mteja aliyefika kwenye Banda lao kupata huduma wakati wa Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yaliyomalizika rasmi jana jumanne Julai 13,2021 Dar es Salaam. (PICHA NA: HUGHES DUGILO.)
Maafisa Usajili wa BRELA wakiendelea na . baada ya kupokea TUZO

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM | Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imeng’ara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yaliyofikia tamati leo Julai 13, 2021 katika Uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere, Dar es Salaam.

Katika maonesho hayo BRELA imeibuka mshindi wa tatu katika kundi la Washiriki wa maonesho hayo wanaojihusisha na Uwezeshaji biashara na Uwekezaji.

Akizungumza baada ya kutangazwa kuwa washindi wa tatu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amebainisha kwamba ushindi huo ni chachu kwa ajili ya kuboresha huduma na kuwafikia watanzania wengi zaidi.

Kwa sasa tunajiandaa na mpango wa kuwafikia wadau wetu waliopo katika Mikoa 16, huu ukiwa ni mwendelezo wa zoezi la kuwafikia wateja wetu popote pale walipo,” alifafanua Bw. Nyaisa.

Alisema pia kuwa BRELA imekwishatoa elimu katika mikoa ya Njombe Singida, Ruvuma, Dodoma, Iringa na Morogoro, lengo likiwa ni kuwafikia wadau katika maeneo yao na kuwahamasisha kuhusu urasimishaji wa biashara na kufanya usajili wa papo kwa papo.

Tangu kuanza kwa maonesho hayo Juni 28, 2021 BRELA imekuwa ikikutana na wadau wake na kuwatatulia changamoto zao papo kwa hapo na kutoa elimu kuhusu huduma zake ili kuwahamasisha Wadau mbalimbali kurasimisha biashara zao.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano BRELA, Bi. Roida Andusamile ameeleza kwamba katika siku 16 za maonesho hayo zaidi ya watu elfu moja walifika katika banda na kupatiwa Elimu za papo kwa papo.

Wadau waliojiandikisha kufika katika mabanda yetu ni 1200 na kati ya hao 618 walipatiwa huduma za papo kwa papo za usajili wa majina ya biashara, usajili wa makapuni, leseni za biashara kundi A na alama za biashara, pia wengine walipata elimu kuhusu huduma zetu na ushauri pia,” alisema Bi. Andusamile.

Maonesho hayo yalizinduliwa rasmi Julai 5, 2021 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na kufungwa na Makamu wa pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here