Home BUSINESS BALOZI RUTAGERUKA AKABIDHI OFISI RASMI KWA NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE BI....

BALOZI RUTAGERUKA AKABIDHI OFISI RASMI KWA NAIBU MKURUGENZI MKUU WA TANTRADE BI. LATIFA KHAMIS


Mhe.Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Edwin Rutageruka akimkabidhi baadhi ya nyaraka za Ofisi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis kwenye hafla ya kumuaga iliofanyika leo tarehe 28 Julai, 2021.

Mhe.Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Edwin Rutageruka akimkabidhi nyaraka za Ofisi Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bi. Latifa Khamis.
 
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis akiongea na Wafanyakazi wa TanTrade wakati wa hafla ya kumuaga Mhe.Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Edwin Rutageruka iliofanyika leo tarehe 28 Julai, 2021 Mkoani Dar es Salaam.
Mhe.Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Edwin Rutageruka akiongea na Wafanyakazi wa TanTrade wakati wa hafla ya kumuaga iliofanyika leo tarehe 28 Julai, 2021 Mkoani Dar es Salaam.

Menejimenti ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Edwin Rutageruka (Katikati)

DAR ES SALAAM.

Mhe.Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasia ya Uchumi Edwin Rutageruka ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) amekabidhi rasmi Ofisi  kwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis katika hafla fupi ya kumuaga  iliyofanyika leo tarehe 28 Julai, 2021 Mkoani Dar es Salaam.

Katika makabidhiano hayo Mhe. Balozi Rutageruka amesema amekuwa na ndoto ya kuifanya TanTrade kuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha mapato ambapo amemuomba Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis kusimamia ukamilishwaji wa miradi ya Maendeleo ambayo ni Kituo cha Nafaka cha Gairo ulipo Mkoani Morogoro, Kilimanjaro Business Park uliopo Mkoani Kilimanjaro, Kurasini Export House uliopo Dar es Salaam, Wajasiriamali Business Centre, mradi wa kuendeleza Uwanja wa Maonesho wa Mwl.J.K. Nyerere (SabaSaba) na kusimamia ujenzi wa mradi wa Uwanja wa Maonesho ya Kimataifa uliopo fumba Zanzibar.

Pia, Mhe. Balozi ameiomba TanTrade kuimarisha Kitengo cha Intelijensia ya Masoko cha TanTrade ambapo kitashirikiana na  Waambata wa Biashara watakao kuwa kwenye Balozi za Tanzania kwenye Nchi mbalimbali na kusimamia miradi ya uwezeshaji biashara Nchini ya Tanzania Trade Information Portal, Tanzania Spice Label na mradi wa E-Shop wa Shirika la Posta kwa kushirikiana na TanTrade.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bi. Latifa Khamis amewaomba Wafanyakazi wa TanTrade kufanya kazi kwa uadilifu na ushirikiano ili kuiwezesha TanTrade kujenga mazingiza wezeshi ya biashara Nchini na kuwataka kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo kusudiwa ya TanTrade na kuahidi kutowavumilia wafanyakazi wavivu na wazembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here