Home LOCAL ASKARI WA JWTZ AKAMATWA KWA TUHUMA NA KUMUUWA KWA KUMPIGA RISASI MWANANCHI.

ASKARI WA JWTZ AKAMATWA KWA TUHUMA NA KUMUUWA KWA KUMPIGA RISASI MWANANCHI.

Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha Justine Masejo
Mganga mkuu wa hospital ya mkoa wa Arusha(Mount Meru)Dokta Alex Ernest akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake(Happy Lazaro).  
 
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Jeshi la polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia Askari wa jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) wa chuo Cha mafunzo ya Kijeshi  Wilaya ya Monduli(TMA) Mkoani Arusha  kwa tuhuma za mauaji ya  Lais Lemomo.
 
 Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha Justine Masejo akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake ,  amesema limetokea baada ya mwanajeshi huyu kumpiga risasi Lemomo akiwa anachunga Mifug.
 
Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na upelelezi pindi utakapokamilika taarifa kamili  zitatolewa.
 
“Tukio hili lilitokea mnamo tarehe 12 mwezi huu majira ya jioni timu ya makachero ipo katika eneo la tukio na uchunguzi utakapokamilika taarifa zaidi itatolewa  “amesema.
 
Mkuu wa wilaya ya Monduli,Frank Mwaisumbe na Mwenyekiti wa halmashauri ya Monduli,Isack Joseph walifika eneo la mauwaji hayo ambapo kumekuwa na mgogoro baina ya wafugaji na Jeshi.
 
Mwaisumbe alitoa pole Kwa familia na kuahidi uchunguzi wa tukio hilo itafanyika na Mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani.
 
Katika hatua nyingine ACP Justine Maseli amesema jeshi la polisi linaendelea kumhoji mganga Mmoja wa kienyeji  mkazi wa kata ya Sombetini kwa tuhuma za kumshawishi  baba wa mtoto kumfanyia ukatilii dhidi ya mtoto wake.
 
“Mnamo tarehe nane mwezi wa saba mwaka huu tulitoa taarifa kuwa  mtoto mwenye umri wa miaka minne alifanyiwa ukatili wa kipigo pamoja na kuwekewa majani mdomoni na baba yake wa kufikia na mwishoni kutelekezwa”ameongeza .
 
Kamanda Masejo amesema baada ya kumkamata na kumhoji mganga huyo alikubali kuwa kweli alimshawishi baba huyo kufanya hivyo na kumwambia endapo angefanya hivyo angepata utajiri katika shughuli zake anazozifanya .
Credit – Fullshangwe Blog.

 

Previous articleMKURUGENZI MTENDAJI NIC APOKEA TUZO YA MSHINDI WA KWANZA WATOA HUDUMA BORA ZA BIMA
Next articleTAASISI NA VYUO VIKUU WEKEZENI KWENYE TAFITI ZA DAWA ZA TIBA ASILI:DKT.GWAJIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here