Home LOCAL ZIARA YA MHE DKT, DUGANGE JIMBONI WANGING’OMBE MEI 21 HADI 23, 2021...

ZIARA YA MHE DKT, DUGANGE JIMBONI WANGING’OMBE MEI 21 HADI 23, 2021 BILIONI MOJA NA MILIONI 500 ZAUNGA MKONO MIRADI YA MAENDELEO



Na Maiko Luoga Njombe

Mbunge wa Jimbo la wanging’ombe Mkoani Njombe na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt, Festo Dugange amefanya ziara  ya siku tatu Jimboni humo kuanzia mei 21 hadi 23 mwaka huu kwa lengo la kuhamasisha, kukagua na kuunga mkono miradi ya maendeleo wilayani Wanging’ombe.

Akiwa kwenye ziara hiyo Mhe, Dugange alibaini uwepo wa changamoto ya ukosefu wa shule za Sekondari za Serikali katika Kata za Kidugala, Malangali na Uhenga, upungufu wa Mabweni, Mabwalo, Madarasa, Majengo ya utawala na vyoo katika shule nyingi za Sekondari wilayani  Wanging’ombe.

Mwezi machi 2021 Mhe, Dugange aliahidi kushirikiana na Serikali kutafuta fedha kwaajili ya ujenzi wa miundombinu ya Elimu na Afya ili kuwapunguzia changamoto Wananchi jambo ambalo Serikali sikivu ya Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha hizo kiasi cha Tsh, Bilioni 1 na Milioni 500 kuunga mkono shughuli za maendeleo.

Baadhi ya maeneo yaliyonufaika na fedha hizo ni pamoja na ujenzi wa Madarasa, Maabara na Jengo la Utawala katika Shule ya Sekondari Ihanga Kata ya Itulahumba iliyopewa kiasi cha shilingi Milioni 100, Shule ya vipaji maalumu ya Wavulana Isatu Kata ya Itulahumba iliyopewa kiasi cha shilingi milioni 80 kwaajili ya ujenzi wa bweni.

Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Vipaji maalumu Maria Nyerere iliyopo Kata ya Wangama imepewa kiasi cha milioni 100 kwaajili ya ujenzi wa bwalo la chakula na Shule ya Sekondari mpya Kata ya Kidugala imepokea kiasi cha shilingi milioni 121.

Shule ya Sekondari mpya Kata ya Malangali imepewa kiasi cha shilingi Milioni 121 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, vyoo na nyumba mbili za watumishi, Shule ya Sekondari mpya Kata ya Uhenga imepewa kiasi cha shilingi Milioni 91 kwaajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu 10 ya vyoo.

Shule ya sekondari Usuka imepokea kiasi cha Tsh, Milioni 30 kwaajili ya ujenzi wa jengo la utawala, Shule ya Sekondari Philip Mangula imepewa milioni 30 kwaajili ya ujenzi wa bwalo, Shule ya Sekondari Igosi imepewa milioni 80 kwaajili ya ujenzi wa bweni na Shule ya Sekondari Ulembwe iliyopata milioni 80 kwaajili ya ujenzi wa bweni.

Pia Shule ya Sekondari Kijombe imepokea kiasi cha shilingi milioni 80 kwaajili ya ujenzi wa bweni, shule ya  sekondari Igima imepewa Milioni 20 kwaajili ya ukamilishaji wa bweni na shule ya Sekondari Wanging’ombe iliyopewa Tsh, Milioni 20 kwaajili ya ujenzi wa Darasa.

Aidha Kituo cha Afya Kata ya Saja ambacho kimekuwa katika hali ya pagala kwa zaidi ya miaka 12 kimepelekewa Sh. Milioni 520 na ujenzi umeanza, katika kipindi chake cha takribani miezi 7 tangu awe Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe Dkt, Dugange ametafuta fedha takribani TSh. Bilioni mbili ambazo zote zimepelekwa kusaidia Wananchi katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Jimboni.

Katika hatua nyingine Mhe, Mbunge wa Jimbo la Wanging’ombe na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt, Festo Dugange kwa nyakati tofauti amesisitiza matumizi bora yenye thamani ya fedha katika miradi husika na kuonya kuwa hatamvumilia yeyote atakaetumia vibaya fedha kinyume na malengo yaliyokusudiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here