Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abadallah akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara kujadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo leo jijini Dar es Salaam.
Dk. Consolatha Ishebabi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo Wizara ya Viwanda na Biashara akiwasilisha rasimu kwa wadau wa sekta binafsi kabla ya kuanza kwa majadiliano kwa washiriki.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Alfred Mapunda akizungumza jambo katika warsha hiyo.
Irene Mlola Mkurugenzi Mtendaji FSDT akitoa mchango wake katika warsha hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam.
Wadau mbalimbali wa sekta binafsi pamoja na Wizara ya Viwanda na Biashara wakjadili mapitio ya rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo ikiendelea leo jijini Dar es Salaam.
DAR ES SALAAM.
Katika kuhakikisha wafanyabiashara wadogo pamoja na wamiliki wa viwanda vidogo wanapata fursa ya kuweza kufanya shughuli zao kwenye mazingira rafiki na wezeshi, Wizara ya Viwanda na Biashara imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kuweza kufanya mapitio ya Sera inayosimamia shughuli hizo ili kuweza kuzijadili na kufanya marejeo kwa lengo la kuziboresha.
Akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo wa siku uliofanyika Jijini Dar esa salaam Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk. Hashil Abadallah Amesema kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuwezesha Sekta ya Viwanda vidogo, vya kati na Vikubwa kwa kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha wananchi wanashiriki kwenye sekta hiyo.
Amesema kuwa Sekta hiyo ni mtambuka na kila mtu anaweza kuingia kwenye Biashara ndogo au kuanzisha kiwanda kidogo na kuweza kufanya shughuli zake na kwamba kwa kuweka mazingira wezeshi yanayoambata na Sera nzuri kutawafanya watu wengi kunufaika na Sekta hiyo.
”Wizara ya Viwanda na Biashara imeamua kufanya mapitio ya Sera kwa kuanza kuifanyia marejeo ili kuweza kuwa na Sera mpya ambayo inakwenda sambamba na ukuaji wa uchumi”
“Pia kuangalia swala la uanzishwaji wa Viwanda vijijini kwa kuzingatia Sera ya uchumi wa viwanda hasa katika kuwawezesha vijana kuweaza kushiriki kwenye fursa hii” Amesema Dkt.
Ameongeza kuwa Sekta hiyo ikifanya vizuri nchi itaweza kujitegemea kimapato na kiajira kupunguza kwa kiasi kikubwa swala la kusafirisha malighafi nje ya nchi.
|