Home SPORTS WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC YAIPA KICHAPO MBEYA CITY 4-1 DIMBA...

WEKUNDU WA MSIMBAZI SIMBA SC YAIPA KICHAPO MBEYA CITY 4-1 DIMBA LA MKAPA.

DAR ES SALAAM.

Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imeendeleza ubabe wa ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuishindilia mabao 4-1 timu ya Mbeya City Katika dimba Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Mabao ya Simba SC yamefungwa na Rally Bwalya dakika ya 31, Luis Miquissone dakika ya 35, Nahodha John Bocco dakika ya 47 na Clatous Chama dakika ya 86, wakati la Mbeya City limefungwa na Pastory Athanas dakika ya 51.

Simba SC inafikisha pointi 73 baada ya ushindi huo katika mechi ya 29 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi sita zaidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC ambao pia wamecheza mechi mbili zaidi.

Previous articleRAIS SAMIA AMTEUA MRITHI WA KENANI KIHONGOSI
Next articleMAGAZETI YA LEO J.TANO JUNI – 23-2021

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here