Home LOCAL WATUMISHI WA WIZARA KUTOA KERO ZAO KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA- DODOMA

WATUMISHI WA WIZARA KUTOA KERO ZAO KWA WAZIRI DKT. GWAJIMA- DODOMA

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akimkabidhi Cheti cha Utumishi Bora Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria Bw. Merick Luvinga kwenye Banda lililopo ofisi za Wizara jengo la NHIF, Mjini Dodoma mapema leo 18 Juni.

Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akionyesha Cheti cha Utumishi Bora alichokabidhiwa  Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria Bw. Merick Luvinga kwenye Banda lililopo ofisi za Wizara jengo la NHIF, Mjini Dodoma mapema leo 18 Juni.


Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kumkabidhi Cheti cha Utumishi Bora Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria Bw. Merick Luvinga kwenye Banda lililopo ofisi za Wizara jengo la NHIF, Mjini Dodoma mapema leo 18 Juni.

Na: Catherine Sungura, DODOMA.

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kesho 19 Juni, Mwaka huu anatarajiwa kusikiliza kero na malalamiko ya watumishi wa Wizara Kwenye ukumbi wa Wizara mji wa Serikali Mtumba.

Akizungumza wakati wa kuzindua maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma mapema leo mjini hapa, alisema kuwa katika kuadhimisha wiki hiyo, atatumia wasaha huo wa kukutana na watumishi ili kusikiliza kero zao mbalimbali kwa lengo la kuzifanyia kazi.

Katika maadhimisho hayo mwaka huu ni “Kujenga  Afrika  tunayoitaka, kupitia  utamaduni  wa uadilifu ambao unastawisha uongozi wenye maono hata Katika mazingira ya mgogoro.

Aidha, Dkt. Dorothy Gwajima ameweza kumkabidhi Cheti Cha Utumishi Bora Mkurugenzi wa Kitengo Cha Sheria,  Bw.Merick Luvinga Kwenye Banda lililopo ofisi za Wizara jengo la NHIF. 

Dkt.Gwajima amesema Wizara imempatia Cheti hicho kilichosainiwa na yeye pamoja na Katibu Mkuu,  Prof. Abel Makubi ikiwa ni kutambua kazi nzuri anayofanya wizarani pamoja na Taasisi zingine kwani wameshapokea barua mbalimbali kutoka Wizara na Taasisi nyingine ambazo amekua akifanya nao kazi za  kumpongeza Mkurugenzi Luvinga .

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here