Home BUSINESS WASHONAJI VIKAPU NJOMBE WAIOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA SOKO LA UHAKIKA.

WASHONAJI VIKAPU NJOMBE WAIOMBA SERIKALI KUWATAFUTIA SOKO LA UHAKIKA.

Picha ya pamoja ya washonaji vikapu kutoka Mkoani Njombe baada ya kumaliza kushona vikapu hivyo.

Wakina Mama mbalimbali wa Mkoa wa Njombe, wakishona vikapu kwa ajili ya kuviuza ikiwa ni sehemu ya shughuli zao za  kujipatia riziki.

Wakazi wa Kijiji cha Ikando mkoani Njombe wakiandaa nyasi kwa ajili ya kushonea vikapu. 

Wakazi wa Kijiji cha Ikando mkoani Njombe wakikata nyasi kwa ajili ya kwenda kutengenezea vikapu. (Picha na John Dande).

Na: Mwandishi Wetu, NJOMBE.

Washonaji wa vikapu Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Mkoa wa Njombe wameiomba serikali kuwatafutia soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao za vikapu ili kuweza kuleta tija.

Wakizungumza na waandishi wa habari washonaji hao wamesema wanakabiliwa na changamoto ya kukosa soko la uhakika na hivyo kulazimika kuuza bila ya faida.

Mmoja wa washonaji hao akiwemo Maria Muhema (61) mama wa watoto watano mkazi wa kijiji cha Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe,amesema ameanza kazi ya ushonaji vikapu tangu akiwa msichana ili kujipatia kipato lakini soko hilo limekua likizunguuka maeneo yao tu hivyo kushindwa kunufaika kwa sababu ya kuuza kwa mazoea.

“Elimu ya ushonaji vikapu tulifundishwa na mzungu alitokea Njombe mjini na nilianza  tangu nikiwa msichana kipato chake bado ni kidogo,lakini ninavyofikiri tukipata mateja nje ya mkoa wetu tutanyanyuka kiuchumi”amesema Maria.

Alisema kuwa wateja wapo lakini bado malighafi za kutengenezea bidhaa hizo kama nyasi  zimekua changamoto kupatikana.

“Kutengeneza hivi vikapu tunatumia nyasi ambazo zinaota kando ya mto lakini wakati mwengine zinakua mbali hivyo tunalazimika kununua kwa vijana ambao wanatuuzia shilingi 10,000 ambapo ukilinganisha na uuzwaji wake wa kusuasua tunapata hasara”amesema.

Naye Furaha Kilasi (39) mkazi wa kijiji cha Ibumila hlamshauri ya wilaya ya Njombe ni mama watoto watatu amesema suluhisho la bidhaa hiyo kuwa na thamani ni kutafuta soko la nje kwa sababu la ndani halijabadilisha maisha yao.

“Nina watoto ninasomesha kupitia kazi hii lakini tunapata kidogo sana,tunaamini tukipata soko la nje bei ya kikapu itaongezeka….ugumu wa maisha ndio ulionifanya nishone vikapu lakini sasa bei haiendani na uandaaji wake ambapo kikapu kinaanzia shilingi 4000 hii sio nzuri kwetu”amesema Kilasi.

Kwa upande wa Sayuni Kaduma (26) mkazi wa kijiji cha Ikando halmashauri ya wilaya ya Njombe,mama wa mtoto mmoja alianza kushona vikapu tangu akiwa mtoto amesema soko la vikapu sio rafiki kwa sababu bei zake ziko tofauti.

“kwa siku tunashona vikapu kimoja au viwili,bei ziko tofauti soko sio zuri unakuta mteja anakuagiza bidhaa ukimpelekea anaanza kujishushia bei au anakwambia havina ubora wakati huo sapo ulishamtumia pamoja na bei zake”amesema Sayuni.

Pia Sayuni ameiomba serikali kuwaunga mkono kwa kuitambua bidhaa hiyo kwa kuwatafutia soko la nje pamoja na kuwatambua katika mikopo ya halmashauri ya asilimia tano za wanawake.

 Credit – Fullshangwe Blog.

Previous articleMATOKEO YA MICHEZO MBALIMBALI ILIOYOCHEZWA KATIKA MASHINDANO YA UMISSETA LEO JUNI 22, 2021
Next articlePSSSF NA BENKI YA AZANIA ZAZINDUA HUDUMA YA KUWAWEZESHA WANANCHI KUMILIKI NYUMBA NA VIWANJA KWA GHARAMA NAFUU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here