Home BUSINESS WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI FURSA ZA BIASHARA ZILIZOPO SAUD ARABIA – BALOZI MWADINI

WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI FURSA ZA BIASHARA ZILIZOPO SAUD ARABIA – BALOZI MWADINI

BALOZI wa Tanzania nchini Saud Arabia  Jabiri Mwadini Akizunguma kwa njia ya mtandao kutokea Nchini humo Katika mkutano na wafanyabiashara kwenye maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara Jijini Dar es Salaam.

Kaimu Meneja wa uendelezaji wa bidhaa Tan trade Masha Hussein (Kushoto) ni Afisa biashara Mwandamizi tafiti za Masoko Tan Trade Asha Malanga.

DAR ES SALAAM.

Watanzania hususani wafanyabiashara wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara zinazopatikana katika nchi ya Saud Arabia ili kuweza kukuza bidhaa mbalimbali zinazohitajika nchi humo.

BALOZI wa Tanzania nchini Saud Arabia  Jabir Mwadini ameyasema hayo katika mkutano uliofanyika kwa njia ya  mtandao kutokea nchini humo ambapo amesema kuwa Tanzania kuna bidhaa nyingi  zenye Masoko  Saud Arabia.

“Kimsingi hapa saud Arabia kuna fursa nyingi sana hivyo ni watanzania wenyewe hususani wafanyabiashara kuchangamkia kwani mbali na nyama lakini pia kuna bidhaa kama samaki Parachini choroko, ufuta na nyinginezo.” Amesema Balozi Mwadini.

Ameongeza kuwa bidhaa nyingine ambazo zina soko kubwa nchini humo ni   Mbolea na Pembejeo za kilimo, lakini pia vifaa tiba vyote vinapatikana nchini humo Kwa gharama nafuu kabisa .

Kwaupande wake Kaimu Meneja wa uendelezaji wa bidhaa Tan trade Masha Hussein amesema wamekuwa wakiandaa mikutano ya kuwajengea uelewa wadau hususani Wafanyabiashara ili kuzijua fursa ambazo zipo katika masoko.

Ameongeza kuwa kwa upande wa nchini ya Saud Arabia wamepata bahati ya kusema na Wafanyabiashara kuona ni kitu gani ambacho kinaihitajika kwenye Soko la nchi hiyo.

“Mfano Soko la chakula ni kubwa katika nchi za uarabuni na wao kama tandrade wanashirikiana vizuri na zingine ili kuweza kupata fursa za masoko katika nchi za uarabuni hususani Saud Arabia  “Amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here