Home BUSINESS WADAU WA CHAKULA KANDA YA KASKAZINI WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO YA UZALISHAJI,USINDIKAJI ...

WADAU WA CHAKULA KANDA YA KASKAZINI WAKUTANA KUJADILI CHANGAMOTO YA UZALISHAJI,USINDIKAJI NA USAFIRISHAJI HADI KUMFIKIA MLAJI.

Baadhi  ya wazalishaji wa chakula wakiwakatika mjadala wavwadau wa chakula uliofanyika mkoani Arusha.

Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe akifungua mjadala wa wadau wa chakula kanda ya Kaskazini uliofanyika mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa usalama wa chakula kutoka wizara ya kilimo Dkt Honest Kessy akiwasilisha nada katika mjadala huo uliofanyika mkoani Arusha.

Nasieku Kisambu mwakilishi wa shirika la WE-EFFECT akiongeana waandishi wahabari wakati wa mjadala wawadau wa chakula Kanda ya Kaskazini.

NA: NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Wadau wachakula kanda ya Kaskazini wamekutana mkoani Arusha katika mjadala wa mifumo ya chakula kwa lengo kubadishana jinsi dunia inavyozalisha, kula na kufikiri kuhusu vyakula ndani ya muktadha wa agenda ya 2030 ya maendeleo endelevu.

Akifungua mjadala huo Meya wa jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe alisema kuwa mjadala huo utasaidia kukabiliana na changamoto umasikini, utoshelevuwa chakula, utapiamlo, ongezeko la idadi ya watu, mabadiliko yahali ya hewa pamoja na uharibifu wa mali asili.

Alisema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi  za Afrika ambazo zimetia saini makubaliano hayo ya kutekeleza malengo 17 ya maendeleo ya umoja wa mataifa(SDGs) ifikapo mwaka 2030 ambapo ingawa nchi zimefanya jitijada mbalimbali kufikia malengo hayo bado wengi wao hawajaweza kufikia.

“Wizara ya kilimo imepewa jukumu la kuratibu na kuhakikisha wadau wote wa umma na binafsi wanahusika katika mazungumzo haya na kwa niaba ya serikali na washushukuru washirika wetu wa maendeleo na wadau wengine kwa kufanikisha mijadala hii,”Alisema Profesa Mwamfupe.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa usalama wa chakula kutoka wizara ya kilimo Dkt Honest Kessy alisema kuwa mkutano huo unalenga kuangalia mnyororo nzima wa uzalishaji hadi kufikia mlaji ili kuona Kuna changamoto gani na wanamatamanio gani ili kufikia malengo.

“Tunataka kujua kwasasa hivi tunavyofanya uzalishaji wetu, usindikaji na usafirishaji hadi kumfikia mlaji  kuna changamoto gani ambazo zipo ili tuweze kuzitatua na hasa kwa kusikiliza mawazo ya wakulima na wafugaji ili waweze kutuambia hali ilivyo sasa hivi na  wangependa mfumo uwe wa namna gani,” Alisema Dkt Kessy.

Nasieku Kisambu mwakilishi wa shirika la WE-EFFECT alisema kama wadau wa chakula wamekuwamstari wambele katika kusaidia mitando ya wakulima kuhakikisha sauti za wakulima wadogo zinajitokeza katika midahalo hiyo na kutoa mapendekezo yao illi serikali iweze kuzifanyia kazi na kupeleka katika ngazi ya kimataifa.

“Wao ndo wanakutana na changamoto kwahiyo sisi tunahakikisha wanashiriki kikamilifu ili sauti zao zisikike na kupata ufumbuzi kwani wakulima wadogo ndio wazalishaji na wanatulisha kwa asilimia kubwa,” Alisema Bi Nasieku.

Mmoja wa wakulima Magreth Nyange kutoka Karatu alisema kuwa wanaiomba serikali iwasaidie kwa kuwaongezea maafisa ugani pamoja na kuwawezesha katika suala zima la kusafirisha mazao wanayoyazalisha nje ya nchi  kupitia usafiri wa anga ili kuweza kufikia mataifa mbalimbali.

Naye mkulima Cornel Mushi kutoka Hai Kilimanjaro (MVIWAKI) alisema kuwa hasara inapotokea katika suala zima la kilimo inaonekana ni hasara ya mkulima peke yake tofauti na nchi zingine zinazoendelea ambapo wakulima wanalipwa fidia hivyo ameiomba serika pale wakulima wanapokutana na changamoto ya hali ya hewa au wanyama kuvamia na kuharibu mashamba yao walipwe fidia.


LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here