Home LOCAL WAAJIRI SEKTA BINAFSI SASA KULIPA ASILIMIA 0.6 YA MICHANGO YA WAFANYAKAZI KWENYE...

WAAJIRI SEKTA BINAFSI SASA KULIPA ASILIMIA 0.6 YA MICHANGO YA WAFANYAKAZI KWENYE MFUKO WA WCF; SERIKALI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama (MB), akizungumza wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria na Menejimenti ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwenye ofisi za Mfuko huo jijini Dar es Salaam Juni 13, 2021
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma, akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alielezea mafanikio ya Mfuko katika maeneo ya ulipaji wa fidia, mifumo ya kisasa ya TEHAMA katika utoaji huduma, uwekezaji, kupanua wigo wa wataalamu hususan madaktari
Murugenzi wa Uendeshaji WCF, Bw. Anse.im Peter (kushoto) akijibu baadhi ya hoja za wajumbe.

Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini WCF, Dkt. Abdulsalaam Omary akifafanua baadhi ya hoja za WajumbeBaadhi ya Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama(katikati) akijadiliana Jambo na Mkurugenzi MKUU wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma ( kulia), MAKAMU Mwenyekiti wa Kati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na SHERIA, Mhe. Giga na NAIBU KATIBU MKUU Ofisi ya WAZIRI MKUU, Profesa Jamal Adam, wakati wa ziara ya Kamati hiyo kutembelea Ofisi za Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) jijini Dar es Salaam juni 13, 2021.

Na: mwandishi wetu

WAAJIRI kutoka Sekta Binafsi sasa watalipa asilimia 0.6 ya michango ya wafanyakazi wao kwenda Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) badala ya asilimia 1 ya awali kuanzia Tarehe 1/7/2021, WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mheshimiwa Jenista Mhagama (MB), amesema leo Juni 13, 2021 jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakati walipotembelea ofisi za WCF jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo mbalimbali ya Kamati ikiwemo kuwekeza katika mifumo ya TEHAMA na uboreshe mfumo wa tathmini ya madai, alisema waajiri kutoka Sekta ya Umma wataendelea kulipa kiwango cha awali cha asilimia 0.5 

“Mama yetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alipoingia madarakani alitoa maelekezo kwa kila taasisi ya serikali iweke mazingiza mazuri ya kuvutia wawekezaji na kupunguza kero zilizokuwa zinaleta changamoto, bila ya kupoteza muda Ofisi ya Waziri Mkuu imeanza kuchukua hatua, na katika kero kubwa iliyokuwa inawakwaza wawekezaji na waajiri nchini hasa Sekta Binafsi ni ule uwiano wa michango asilimia 0.5 Sekta ya Umma na asilimia 1 kwa sekta binafsi, sasa tumetekeleza kwa kuondoa huo mzigo wa uchangiaji.” Alisema Mheshimiwa Waziri.

Pia Mheshimiwa Waziri alisema sambamba na hilo, Serikali kupitia WCF inafikiria kufuta malimbikizo ya madeni ya michango ya huko nyuma ili  kuwepo kwa mazingira mazuri kwa wale Waajiri ambao hawajajisajili ili waweze kujisajili  na isiwe kikwazo kwao na waliojisaljili watekeleze wajibu wa kulipa michango.

Alisema kipaumbele cha Serikali ni kuimarisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ili uendelee kulipa fidia kwani huduma za hifadhi ya jamii ni haki ya kikatiba.

“Hifadhi ya jamii ni haki ya kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 11(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977. Ibara hii inaipa Serikali wajibu wa kuweka mazingira ya kisera na kisheria kwa lengo la kuhakikisha, pamoja na mambo mengine, kwamba kila mwananchi anapata kinga wakati wa uzee, ugonjwa au ulemavu.” Alifafanua Mheshimiwa Mhagama.

Waziri huyo aliwahakikishia wajumbe hao kuwa ripoti ya mtathmini (Acturial report) imeonyesha kazi ya Mfuko ni nzuri na Mfuko unaendelea vema na kuitaka Menejimenti iendelee kuchapa kazi kwa kujituma na kuweka uzalendo mbele.

“Katika uhai wake wa miaka sita tangu uanzishwe Mfuko umekutekeleza takwa hilo la kikatiba kwa mafanikio makubwa ambapo mwaka 2015-2016 ulilipa Fidida ya Shilingi Bilioni 1.55 na sasa Fidia imefikia hadi shilingi bilioni 9.05.

Kwa upande wake Makamu Mwenyemkiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa Najma Giga alisema, Kamati yake imeridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Mfuko katika kutekeleza maelekezo ya Kamati ambapo hivi sasa huduma za Mfuko zimerahisishwa kufuatia matumizi ya TEHAMA ambapo huduma mbalimbali zinafanyika kidigitali.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma alieleza mafanikio mbalimbali
katika upande wa makusanyo ya michango, mifumo ya kutolea huduma, uwekezaji, malipo ya fidia na katika kipindi chote cha utekelezaji wa majukumu yake, Mfuko umekuwa ukipata hati safi ktoka kwa Mkaguzi Mkuu.

“Pamoja na mafanikio haya pia kuna changamoto kama vile uelewa mdogo, lakini pia waajiri kutowasilisha nyaraka za ukweli na sahihi, lakini pia Mfuko unaelekeza nguzu zake katika kuhakikisha unaondoa changamoto ya madaktari kwa kuendelea kutoa mafunzo nchi nzima.” Alisema Dkt. Mduma.


Previous articleRAIS SAMIA AZINDUA MRADI WA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MISUNGWI MKOANI MWANZA
Next articleMAAFISA UGANI WOTE LAZIMA WAWE NA MASHAMBA DARASA-MAJALIWA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here