Home BUSINESS UZALISHAJI WA NG’OMBE KWA NJIA YA CHUPA MKOMBOZI KWA WAFUGAJI

UZALISHAJI WA NG’OMBE KWA NJIA YA CHUPA MKOMBOZI KWA WAFUGAJI

Msimamizi wa Programu Pendo Kivuyo akimchoma Ng’ombe sindano ya kumpamdisha joto kwa ajili ya uzalishaji kwa njia ya chupa.

Wanufaika wa programu hiyo ambao ni wafugaji kutoka katika kata za Manispaa ya Kahama.

Mitungi maalumu ya kuhifadhia Mbegu kwa ajili ya Uzalishaji

Na: Cymon Mgendi, KAHAMA.

Kanisa la kiinjili  la kilutheri Tanzania (KKKT) Kupitia PROGRAMU YA MAISHA ENDELEVU NA UWEZESHAJI, Limezindua aina mpya ya uzalishaji wa Ng’ombe kwa njia ya chupa,  jambo ambalo litapunguza changamoto ya uzaliwaji wa Madume mengi na kuongeza thamani ya Ng’ombe, kipato pamoja na kumuezesha mfugaji kuchagua Ng’ombe mwenye sifa anazotaka.

Uzinduzi huo umefanyika leo katika Manispaa ya Kahama kwenye Kanisa la KKKT, Jimbo kuu dayosisi ya kusini mashariki ya ziwa Vicktoria, na kuuzuriwa na makundi ya wafugaji yaliopo chini ya mradi huo wa Kanisa  kutoka katika kata za Manispaa ya Kahama, amabazo ni Kinaga, Zongomela,Nyahanga pamoja na Mhongolo.

Mratibu wa Mradi huo wa uzalishaji Ng’ombe kwa njia ya Chupa,  Patricia Mwaikenda, amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuboresha zaidi ambapo mfugaji atapata ndama bora zaidi pamoja na maziwa kuongezeka.

Kwa upande wake mgeni rasimi, katibua tawala Wilaya ya Kahama, Thimos Ndanya, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Anamringi Macha, amelipongeza Kanisa la KKKT  kwa kwakua mradi huo umelenga kuwainua wananchi wa hali ya chini kiuchumi, na kuongeza kuwa serekali itakua pamoja na wao kwa kutatua changamoto zote zinazowakabili.

Nao baadhi ya wa fugaji Ambao watanufaika na Mradi huo Lucia Kafumu na Agustino Magema wamesema kuwa Mradi huo utakwenda kuondoa Changamoto walizokua wanazipata hapo awali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here