Home BUSINESS TBS YAWAFUNDA MAWAKALA WA FORODHA NA WAFANYABIASHARA WA MAHINDI MPAKANI HOROHORO TANGA

TBS YAWAFUNDA MAWAKALA WA FORODHA NA WAFANYABIASHARA WA MAHINDI MPAKANI HOROHORO TANGA

Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga akisistiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga Mkoani Tanga ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi kushoto ni Meneja wa TBS Kanda ya Kaskazini Happy Brown.
Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga akisistiza jambo wakati akifungua mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga Mkoani Tanga ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi

Dkt.Candida Shirima kutoka TBS akitoa mada wakati wa semina hiyo kuhusu
Sumu kuvu,Visababishi,Madhara yake na namna ya kuhifadhi Mazao kushoto ni Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga

TANGA.
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa Mawakala wa Forodha na Wafanyabiashara wa mahindi na nafaka nyengine katika mpaka wa Horohoro wilayani Mkinga Mkoani Tanga ikiwa ni kuwapa elimu ya namna taratibu zinazotakiwa kufuatwa wakati wa kusafirisha mahindi kwenda nje ya mipaka nchi.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Lazaro Msasalaga amesema wafanyabiashara hawana budi kuhakikisha mahindi wanayonunua kama yamezingatia kanuni bora za kulimo ili kuzuia fangasi wanaoweza kusababisha sumu kuvu kwenye mahindi.

Alisema wafanyabiashara hao wanatakiwa kujua mahindi wanayokuwa wakinunua yanayotoka wapi ili kuweza kuepuka hasara inayoweza kujitokeza pindi mahindi yatakapokuwa na sumu kuvu.

“Ni muhimu sana kwa wafanyabiashara kujua Mahindi wanayoyanunua yanazalishwaje kwani ni muhimu sana kujua yule anayekuuzia mahindi kwa lengo la kujua kama anafuata kanuni bora za kilimo kutokana na kwamba inakupa uhakika na ukinunua haitaleta shida kwenye usafirishaji”Alisema Msasalaga.

“Mafunzo haya yatawasaidia wafanyabiashara namna ya mahindi yanavyopokelewa,kuna taratibu za kupeleka mahindi nje ya Nchi na kila Nchi ina namna ya kulinda usalama wa wananchi wake”alisema Msasalaga.

Akielezea namna ya sumu kuvu iweze kuepukika,Msasalaga amesema ni lazima kanuni bora za usindikaji wa mahindi na mnyonyoro mzima wa uzalishaji uwe umefuatwa huku akiwataka wafanyabiashara wafuate taratibu ambazo zinatakiwa kwa kuwa nchi inayopokea bidhaa ndio inayotoa sharti ya kupokea mizigo.

Semina hiyo inafanyika katika Mikoa mitatu yenye Mipaka ya Holili mkoani Kilimanjaro,Namanga Mkoani Arusha na Horohoro Mkoani Tanga

Previous articleRAIS SAMIA AWATAKA WANAWAKE WOTE NCHINI KUTOJIONA WANYONGE.
Next articleSERIKALI YASISITIZA MIONGOZO YA YA KUJIKINGA NA COVID-19 IZINGATIWE

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here