Home SPORTS SIMBA FC YATINGA FAINALI KOMBE LA FA, YAICHAPA AZAM FC 1-0 DIMBA...

SIMBA FC YATINGA FAINALI KOMBE LA FA, YAICHAPA AZAM FC 1-0 DIMBA LA MAJIMAJI SONGEA.

SONGEA.

Timu ya wekundu wa Msimbazi Simba SC imefanikiwa kutinga  hatua ya Fainali ya Kombe la Azam Federation Cup (FA) kwa kuichapa Azam FC bao 1-0 katika dakika za lala salama za mchezo huo uliopigwa katika Dimba la Majimaji Mjini Songea.

Mshambuliaji wa Kimataifa Luis Miquiaonne alipachika bao la kuongeza na la ushindi kwa mkwaju mkali baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa kuingo Mshambuliaji Bernald Morrison kufuatia mpira wa adhabu nje kidogo ya eneo la penati.

Kufuatia ushindi huo sasa timu ya Simba itaumana na timu ya Yanga katika hatua ya Fainali mchezo utaokaochezwa Julai 25-2021 Mjini Kigoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here